Uchangishaji fedha wa 2012/Tafsiri/Barua ya Jimmy

This page is a translated version of the page Fundraising 2012/Translation/Jimmy Appeal and the translation is 100% complete.

NOTE TO TRANSLATORS

This letter is a new translation request, but re-uses large parts of the 2011 Jimmy Appeal, with slight modifications in the second version.

https://meta.wikimedia.org/wiki/Fundraising_2011/Jimmy_Letter_002/en

If the 2011 Jimmy Letter has been translated into your language, you can probably re-use much of it for this translation. :-) Jseddon (WMF) (talk) 18:37, 27 September 2012 (UTC) [reply]

Version 1 (Millions)

Pengine Google ina mashine za seva karibu milioni 1, Yahoo wana wafanyakazi 12,000. Sisi katika Wikipedia tuna seva 800 na wafanyakazi 150.

Wikipedia ni tovuti ya tano duniani kwa hesabu ya kutembelewa. Kila mwezi watu milioni 450 hutembelea tovuti yetu – wakiangalia mabilioni ya kurasa zetu.

Si vibaya kufanya biashara au kuonyesha matangazo ya kibiashara – lakini hapa si mahala pake. Siyo katika Wikipedia.

Wikipedia ni kitu maalumu. Ipo kama maktaba au mahali pa umma. Pako kama hekalu la maarifa. Ni mahali ambapo wote twaweza kwenda na kutafakari, kujifunza, na kuwagana maarifa yetu na wengine.

Nilipoanzisha Wikipedia ingekuwa rahisi kuijenga kama biashara na tovuti inayozalisha pesa nyingi kwa njia ya kuonyesha matangazo ya kibiashara. Lakini sikutaka. Kwa hiyo tumejenga Wikipedia kwa pesa kidogo hasa kwa kujitolea na zawadi za wachangiaji. Usimamizi wa mitambo unaendeshwa na watu wachache sana. Ofisi ya Wikipedia haikuweza kunenepa – wanenepe wengine!

Kama kila msomaji angetoa $5 kila mwaka kwa matumzi yake ya Wikipedia tusingehitaji kuomba kitu. Lakini si wote wanaoweza au wanaotaka kujitolea kwa njia hii. Hata hivyo tumepata wasaidizi wa kutosha hadi sasa.

Kwa sababu hii ninakuomba: usaidie na wewe mwaka huu. Ujitolee kwa dola 5, 10, 100 au jinsi unavyoweza. Tuendelee kujenga Wikipedia.

Ahsante sana,

Jimmy Wales
Mwanzilishi wa Wikipedia

Version 2 (Thousands)

Google na Yahoo zina maelfu ya seva na wafanyakazi. Sisi tuna seva kama 800 na wafanyakazi kama 150.