Fundraising 2010/Appeal/sw


Miaka 10 iliyopita watu wengi walinitazama kama kioja nilipoanza kuongea na watu kuhusu Wikipedia.

Walikuwa na mashaka kama wanamtandao wa kujitolea kutoka pande zote za dunia wangeweza kushirikiana na kukusanya ujuzi wa ubinadamu wakilenga kushirikiana tu.

Bila matangazo ya kibiashara. Bila nia za siri. Bila masharti yoyote kwa watumiaji.

Miaka 10 baada ya vyanzo vile kuna watu milioni 380 wanaotumia Wikipedia kila mwezi - hao ni takriban theluthi moja ya watu wote waliounganika na mtandao dunani.

Wikipedia ni tovuti maarufu ya tano duniani. Tovuti nne zingine kubwa zimejengwa na kuendelezwa kwa uwekezaji wa mabilioni ya madola, ushirika mkubwa wa wafanyikazi na kwa kutangaza kwa sauti mno.

Lakini Wikipedia si mradi wa kibiashara. Inajengwa na jumuiya yake ambao ni watu wanaojitolea kuchangia. Wewe u mmoja wao katika jumuiya hii. Mimi ninakuandikia barua hii siku ya leo kwa kukuomba ulinde na udumishe Wikipedia.

Sote pamoja tunaweza kuitunza kama mahali pasipo na malipo kwa watumiaji na pasipo na matangazo ya kibiashara. Tunaweza kuitunza kama tovuti huria - mtu yeyote yu huru kutumia elimu iliyomo katika Wikipedia jinsi anavyopenda. Kwa njia hii tunaendelea kuikuza: tunasambaza elimu tukiwakaribisha wote wapate kuchangia.

Kila mwaka wakati huu tunapiga hodi kwako na kwa wote wengine katika jumuiya ya Wikimedia kwa ombi la kuchangia kwa mradi wetu wa pamoja: $ 10, 30, 50 au zaidi.

Ukipenda Wikipedia kama chanzo cha habari na elimu natumaini utachukua hatua inayofaa.

Ndimi wako

Jimmy Wales

Mwanzilishaji wa Wikipedia.

Nyongeza: Wikipedia imejengwa na watu wanaoshirikiana katika kujenga kitu cha ajabu. Watu kama sisi wenyewe waniandika Wikipedia neno kwa neno. Watu kama sisi wenyewe wanachangia mahitaji ya mradi mchango kwa mchango. Hii ni jinsi tunavyojenga uwezo wa pamoja kubadilisha dunia.