Kamati ya uchaguzi ya shirika la Wikimedia 2013
The election ended 22 June 2013. No more votes will be accepted. The results were announced on 24 June 2013. |
Kamati ya uchaguzi wa Bodi 2013 inasimamia mwenendo wa uchaguzi kwa kadri ambavyo imepewa mamlaka na Baraza la udhamini,subject to Board overview, na itatoa mapendekezo kwenye baraza kuhusiana na suala zima la Uchaguzi.
Uanachama
Kamati inajumuisha wajumbe walioteuliwa na board of trusteeskuandaa Uchaguzi wa Baraza la wadhamini la Wikimedia. wajumbe wa Kamati lazima wawe ni wahariri wa mradi mmojawapo wa miradi ya Wikimedia, asiwe ni miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Udhamini ama mgombea wa Uchaguzi na haruhusiwi kupiga kura katika Uchaguzi.
iliyotangazwa tarehe 5, february 2013, wajumbe wa kamati walikuwa kama ifuatavyo:
Jina | Lugha | Mahali (ukanda wa majira) |
---|---|---|
Ferdinando Scala | it, nap, en-5, fr-5, es-2 | San Giorgio a Cremano, Italy (UTC+1) |
Jon Harald Søby | nb, en-3, sv-3, de-2, da-2, es-1, eo-1, ro-1, sw-1 | Trondheim, Norway (UTC+1) |
Katie Chan | en, yue | Lincoln, England (UTC+0) |
Ralf Roletschek | de, es-2, ru-1, cs-1, ca-1, en-0 | Eberswalde, Germany (UTC+1) |
Risker | en, fr-2 | Toronto, Canada (UTC-5) |
User:Philippe(WMF)philippe Beaudette alihudumu kama mjumbe msaafu, pamoja na Geoff Brigham ambaye husaidia katika masuala ya kisheria.
Masuala
Kamati ina wajibu wa kupanga na kusimamia masuala yote ya husianayo na Uchaguzi wa Bodi, kwa mfano, kamati hupanga namna ya upigaji kura, na vigezo vya namna ya kugombea, kuandaa rasimu maalum wa Uchaguzi kwenye ukurasa wa Meta, kujiridhisha kwamba wagombea na wapiga kura wametimiza vigezo vinavyohitajika, kukagua kura na kuhakikisha kwamba hakuna kura ambazo zimepigwa kinyume pamoja na matizo mengine.