Mpango wa Mwaka wa Shirika la Wikimedia Foundation

This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan and the translation is 98% complete.

Mpango wa Mwaka wa Shirika la Wikimedia Foundation ni mpango wa kazi za Wikimedia Foundation za kila mwaka. Kazi hizi zinapangiliwa kwa mwaka mzima wa fedha wa Shirika la Wikimedia Foundation, utakaoanza Julai 1 na kumalizika Juni 30 mwaka unaofuata. Uundaji wa mpango wakati mwingine unaweza kujulikana kama Mchakato wa Upangaji wa Mwaka au APP.

De Groene Verbinding
De Groene Verbinding

Orodha ya mipango ya mwaka


Maswali yaulizwayo Mara Kwa Mara (FAQ)

  1. Mpango wa kila mwaka ni nini?
    Mpango wa kila mwaka ni ramani ya ujumla juu ya kile ambacho shirika linalenga kutimiza katika mwaka ujao. Kwa kawaida huainisha vipaumbele muhimu, mahitaji ya rasilimali, na matokeo yanayotarajiwa ambayo yameundwa pamoja na Harakati za Wikimedia, na matokeo hayo yanaendana na mfumo mpana wa ahadi zetu za miaka mingi na mwelekeo wa kimkakati wa Harakati za Wikimedia.
    Katika Shirika la Wikimedia Foundation, mpango wa kila mwaka unakusudiwa kutoa mwongozo wa mwelekeo kwa wasimamizi na timu kwa kuunda miradi wanayofanyia kazi mwaka mzima. Haikusudiwi kuwa orodha ya miradi ya vipengele vya kiufundi, kwani hivyo hubadilika mwaka mzima. Mpango wa kila mwaka una vipaumbele na dhana za kiwango cha juu ambazo huongoza timu kufanya utafiti, kubuni, kujaribu na kupeleka mikakati tofauti. Hadhira kuu ya mpango wa mwaka ni idara za ndani, timu, na wafanyakazi binafsi wanaoutumia kuongoza kazi zao mwaka mzima, ambayo inaonekana katika toni ya mpango, lugha na muundo. Inaundwa kwa ushirikiano na kuwekwa hadharani kila mwaka kwanza katika fomu ya rasimu na kisha kama bidhaa ya mwisho ili kutoa uwazi na kuomba maoni kutoka kwa Wanawikimedia.
  2. Je, sehemu kuu za mpango wa mwaka ni zipi?
    Kuanzia mwaka wa fedha wa 2023-2024, Shirika lilianza kuchapisha sehemu mahususi za maeneo manne ya malengo makuu yaliyojikita katika mwelekeo wa kimkakati: Miundombinu, Usawa, Usalama na Uadilifu, na Ufanisi. Mpango wa kila mwaka pia hujumuisha maelezo kuhusu mitindo mikuu ya nje ambayo inaweza kuathiri kazi yetu, pamoja na shughuli zetu, kazi za idara, bajeti, utoaji ruzuku na mifumo ya mapato.
  3. Kwa nini Shirika lina mpango wa kila mwaka?
    Mpango wa kila mwaka husaidia Shirika la Wikimedia Foundation kuunganisha shughuli ambazo wafanyakazi hufanya kila siku kwa dhamira yetu na maono mapana, kile ambacho ulimwengu unahitaji kutoka kwetu, pamoja na mwelekeo wa kimkakati wa Wikimedia. Ni wakati ambapo viongozi wa Shirika hupima vipaumbele shindani vya jinsi timu zao zinapaswa kutumia muda katika mwaka ujao, na kuhakikisha kwamba tunakidhi mahitaji changamano na yanayoendelea ya wasomaji, wachangiaji, wafadhili na jukwaa letu. Pia huwapa wafanyakazi katika Shirika fursa ya kujiridhisha na vipaumbele hivi na kuboresha njia za kufanya kazi na wafanyakazi wa kujitolea, washirika, Baraza la Wadhamini, na kila mmoja katika timu na idara.
  4. Je, muda wa mpango wa mwaka ni upi?
    Wikimedia Foundation linafuata kalenda ya fedha ya Julai-Juni. Hii inamaanisha kuwa mwaka wa fedha (FY) 2024-2025 unajumuisha Julai 2024 hadi Juni 2025. Katika mwaka huo, kwa kawaida tunafuatilia kazi yetu katika robo-mwaka nne, kila moja kwa muda wa miezi mitatu.
  5. Je, mpango wa mwaka unaandikwaje?
    Mchakato hubadilika mwaka hadi mwaka, lakini katika miaka michache iliyopita tumeendelea kukua na kuboresha mchakato wa upangaji shirikishi.
    Majadiliano ya Mwaka wa Fedha wa 2024-2025 yalianza na Mazungumzo:2024 - mazungumzo kati ya wafanyakazi wa Shirika, viongozi, wanachama wa bodi, na Wanakimedia duniani kote. Maoni kutoka kwenye mazungumzo haya yalitoa picha ya vipaumbele vilivyowekwa chini ya malengo ya mpango wa mwaka. Mazungumzo:2024 yalifuatiwa na mwaliko kutoka kwa Afisa Mkuu wa Bidhaa na Teknolojia Selena Deckelmann kwa maoni kwenye wiki katika malengo yanayopendekezwa kwa ajili ya kazi ya bidhaa na teknolojia ya Shirika mwaka ujao. Malengo haya yanatokana na mazungumzo yanayoendelea kupitia Mazungumzo:2024, ambayo yaliangazia umuhimu wa kuendelea kuzingatia mahitaji ya mfumo wetu na wachangiaji mtandaoni. Matokeo muhimu ya Bidhaa na Teknolojia yalichapishwa mwishoni mwa Machi, na haya yalifuatwa na nyenzo kamili za mpango wa mwaka tarehe 11 Aprili 2024.
    We welcomed ideas over a two-month period on-wiki, in community channels and through live discussions in co-created community spaces in many languages. Wikimedians shared their take on the proposed plans and about their own goals for the upcoming year. Inspired by what so many others are doing in their own work, we continue to find opportunities to collaborate and learn from the planning processes and work of others in the Wikimedia movement as well as other partners. Throughout the period changes were made to the plan - see edit histories and a summary of feedback, engagement statistics and changes to the annual plan will be available over the next few weeks like in previous years. As the annual plan is not meant to be a list of projects or technical features, which evolve throughout the year some of the conversations started during the annual plan will continue to be live conversations.
  6. Ni nini kinaunda kile kinachoingia katika mpango wa mwaka?
    Kuna mambo kadhaa yanayounda kile kinachoingia katika mpango wa kila mwaka wa Shirika la Wikimedia Foundation. Tunaanza kwa kufikiria "ulimwengu unahitaji nini kutoka kwetu"? Hii inamaanisha kuangalia mienendo ya kimataifa, kama vile kuongezeka kwa taarifa potofu na taarifa za uzushi, akili bandia, mabadiliko ya mitindo ya utafutaji, na mabadiliko ya kimataifa ya kisheria.
    Jambo linalofuata tunalofikiria ni "watazamaji wetu wanahitaji nini kutoka kwetu?" Katika kiwango cha msingi sana, hadhira yetu inajumuisha wachangiaji, wasomaji na wengine wanaotumia maudhui yetu, na wafadhili. Kwa wachangiaji, tunamaanisha mtu yeyote anayetoa muda wake kukuza au kuboresha maudhui kwenye miradi ya Wikimedia ikiwa ni pamoja na wahariri (wa viwango vyote vya uzoefu), wanaopakia maudhui na wasanidi wa kujitolea. Aina ya pili inajumuisha kila mtu kutoka kwa wasomaji binafsi hadi watafiti wa kitaaluma hadi mashirika makubwa ambayo hutumia na kutumia tena maudhui ya Wikimedia. Kwa wafadhili, tunamaanisha mtu yeyote anayetoa usaidizi wa kifedha wa ukubwa wowote na kupitia njia yoyote. Tunatafakari kile tunachosikia mwaka mzima kutoka kwenye Harakati za Wikimedia kuhusu mitindo ya kimataifa ambayo tunapaswa kuzingatia, mahitaji ya miundombinu na programu, changamoto za kisheria na udhibiti, na kile ambacho ulimwengu unapaswa kujua kuhusu kazi yetu ya pamoja.
    Hatimaye, sehemu muhimu ya mpango wa kila mwaka ni kile ambacho hakipo katika mpango. Wakati wa kupanga kila mwaka, wafanyakazi wa Shirika na viongozi wanapaswa kupima mabadiliko muhimu kuhusu mustakabali wa bidhaa na programu zetu. Sehemu ya hii ni kwa sababu tunapandisha bajeti yetu ya uendeshaji ya kila mwaka kila mwaka; kimsingi, tunaweza kutumia kile tunachochangisha katika mwaka fulani, huku kiasi kidogo cha jumla ya fedha zilizokusanywa zikienda kwenye hifadhi zetu za kifedha (kwa matukio yasiyotarajiwa) na Waraka wa Wikimedia (kwa mapato thabiti zaidi ya muda mrefu). Tunachoweza kupangilia huchangiwa na makadirio ya bajeti na mapato kwa mwaka, pamoja na kujitolea kwetu kudumisha uwiano thabiti wa gharama za programu.
    Kwa baadhi ya watu, kuwepo kwa mabadiliko ya matumizi kunaonekana kutowezekana kwa kuzingatia ukubwa wa bajeti yetu ya kila mwaka, lakini kama wapangaji inabidi tufikirie kwa vitendo jinsi bajeti yetu inavyotumika kusaidia miundombinu ya kiufundi ambayo tunaweza kuitunza. Kwa lenzi hii, Shirika la Wikimedia Foundation ni la kipekee: hakuna mashirika mengine makubwa ya kiufundi duniani yenye ukubwa wa trafiki ya tovuti, nyayo za mtandaoni, uwezo wa lugha nyingi na utumiaji upya wa data ambao hufanya kazi kwa bajeti isiyo ya faida na hawaonyeshi matangazo au kuuza data zako. Kwa hivyo, maswali tunayofikiria kwa kawaida sio "ni nini kinahitaji kurekebishwa?" lakini “ni fursa gani muhimu au tatizo gani la kuzingatia mwaka huu? Je, timu zetu zinaweza kuwa na matokeo ya maana katika eneo hilo kwa rasilimali tulizonazo?”
  7. "OKRs" na "Dhana" ni nini?
    Tulianza kutumia lugha hii ya kupanga kwa uthabiti zaidi katika mpango wa mwaka wa fedha(FY) wa 2023-2024, na tutaendelea kufanya hivyo kwa siku za usoni zijazo .
    Upangaji mzuri wa kimkakati unamaanisha kuanza na athari au mabadiliko tunayotarajia kufanya - mambo kama vile kufanya maudhui ya Wikimedia kugundulika zaidi, kupunguza muda wa upakiaji wa ukurasa katika sehemu fulani ya dunia, kuongeza uhifadhi wa watumiaji wapya, kuboresha mtiririko wa msimamizi, au kuyalinda dhidi ya aina fulani ya tishio la kisheria. Mambo haya yanaonyeshwa kama “malengo”, au taarifa inayonasa athari pana tunayotarajia kufikia.
    Hatua inayofuata ni kubainisha kauli kadhaa zinazoweza kupimika ambazo zingetusaidia kufikia malengo hayo mapana na kabambe. Haya yanajulikana kama "matokeo muhimu" na yanawakilisha njia za kiwango cha juu ambazo tunaweza kuonyesha kwa njia inayopimika ikiwa tumetimiza malengo yetu. Kuanzia hapo, tunaunda dhana ili kuwakilisha jinsi timu zinavyoamini kuwa zinaweza kuchangia katika kufanikisha Malengo Muhimu(KR). Dhana ni pale tunapotekeleza kazi ya kina inayohitajika ili kufikia malengo yetu. Taarifa kuhusu dhana hupatikana kwenye kurasa za mradi za timu binafsi.
    Hatimaye, OKR hazikusudiwi kunasa kila kitu tunachofanya. Kuna kazi nyingi zinazoelekezwa kwa matengenezo ambazo wafanyakazi wa Shirika la Wikimedia Foundation hutumia muda mwingi kwa mwaka mzima, ikijumuisha usimamizi wa chapa ya biashara na chapa, matengenezo ya programu na kurekebisha hitilafu, kutegemewa kwa tovuti na usalama, na mahusiano ya umma na usimamizi wa sifa.
  8. Kwa nini kila kitu kinasikika kama hakipo wazi?
    Mpango wa kila mwaka unaonesha kwa upana kile tunachotarajia kubadilisha au kufikia katika mwaka fulani wa fedha. Mara tu vipaumbele hivyo vinapowekwa, timu za Shirika hutumia mwaka kutafakari jinsi ya kufikia mabadiliko hayo, kama vile kipengele kipya cha bidhaa, mfumo wa data, utendakazi wa uhandisi, mkakati wa kisheria, kampeni ya mawasiliano, au mpango wa jumuiya, na kisha kuutekeleza.
  9. Je, Shirika la Wikimedia hutathmini na kushirikisha vipi maendeleo na athari?
    Mpango wa kila mwaka unajumuisha sehemu ya vipimo ambavyo tunatumia kupima athari na maendeleo yetu dhidi ya mpango huo. Tunachapisha habari hii mara kwa mara. Tazama mifano ya zamani katika chapisho la Diff "Kuimarisha Muunganisho katika Harakati za Wikimedia" na sasisho kuhusu maendeleo dhidi ya mpango wa 2023-24 katika chapisho la Diff "Maendeleo kwenye mpango: Jinsi Shirika la Wikimedia Foundation lilivyoendeleza malengo yake ya Mpango wa Mwaka".
  10. Je, mpango wa mwaka ni sawa na ripoti ya mwaka?
    Hapana. Mpango wa mwaka ni hati ya mipanga ya kazi iliyokusudiwa kwa mwaka ujao. Hadhira kuu ya waraka huu ni wafanyakazi, pamoja na watu wa kujitolea, wafadhili, na wasomaji. ripoti ya mwaka ni hati tangulizi inayokusudiwa kuangazia athari zetu kwa ulimwengu, na hadhira yake kuu ni wafadhili na umma kwa ujumla.

Tazama pia