Chaguzi za Shirika la Wikimedia/2022
Wakati wa uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ya mwaka 2022, wagombea wawili wa jumuiya na washirika watachaguliwa kuhudumu katika Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia. Ukurasa huu una muhtasari wa uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ya mwaka 2022.
The elected candidates were:
You may also view the full results, including the outcome of each round of Single-Transferrable Vote.
Kuhusu uchaguzi
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia inasimamia shughuli za Shirika la Wikimedia. Wadhamini wa jumuiya na wadhamini walioteuliwa wanaunda Bodi ya Wadhamini. Kila mdhamini anahudumu kwa muda wa miaka mitatu. Jumuiya ya Wikimedia ina fursa ya kuwapigia kura wadhamini waliochaguliwa na jumuiya na washirika. Wagombea wawili watajiunga na [Bodi ya Wadhamini]. Wagombea waliochaguliwa wataorodheshwa kwanza na washirika na hatimaye kuchaguliwa na jumuiya.
Ujuzi na uzoefu unaohitajika
Wikimedia ni harakati ya ulimwengu na Bodi inatafuta wagombea kutoka katika jumuiya pana. Wagombea wanaofaa ufungamana na dhamira ya Wikimedia na wanafikra, heshima, na mwelekeo wa jumuiya.
Bodi ingependa kupata mitazamo na sauti ambazo zina uwakilishi mdogo na muhimu kwa harakati zetu. Ili kujaza mapengo katika uwakilishi wa kihistoria na wa sasa ndani ya Bodi, Bodi ya Wadhamini inatarajia kuhimiza maombi hasa kutoka kwa wale walio na uzoefu katika maeneo yafuatayo: Afrika, Asia ya Kusini, Mashariki na Asia ya Kusini-Mashariki na Pasifiki, na Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibi. Uzoefu unaohitajika wa kikanda sio hitaji, lakini sababu ya ziada. Badala ya kuwa wa lazima, hizi ni sifa muhimu ambazo Bodi inasihi kila mtu azingatie.
Bodi inaelewa kuwa kuna uwezekano kwamba baadhi ya wagombea kutoka maeneo yaliyonyimwa kipaombele huleta mtazamo bora zaidi juu ya utofauti kuliko wagombea wengine kutoka maeneo yaliyopewa kipaumbele ambao hawajui masuala ya usawa. Wagombea wanapaswa kushiriki jinsi uzoefu wao umewawezesha kukuza utofauti, usawa, na ujumuisho.
Ujuzi
Maeneo ya uzoefu ambayo Bodi imetaja kuwa na manufaa zaidi kwa wadhamini wapya kuleta ni:
- Mkakati wa shirika na usimamizi
- Teknolojia ya jukwaa la kiwango cha biashara na/au ukuzaji wa bidhaa
- Sera ya umma na sheria
- Sayansi ya data jamii, uchambuzi mkubwa wa data, na kujifunza kwa mashine
Pata maelezo zaidi kuhusu mitazamo, uzoefu na ujuzi unaohitajika kwa wagombea kuwa nao katika uchaguzi huu kwenye ukurasa wa Omba kuwa Mgombea.
Upigaji kura wa jumuiya
Wanajamii watapata fursa ya kupiga kura kuchagua wadhamini wawili kati ya wagombea sita walioteuliwa na washirika. Kura Moja Inayohamishika kwenye KuraSalama itatumika mwaka huu.
Baadhi ya wanajamii walibainisha kuwa ilikuwa changamoto katika kuchagua watahiniwa mwaka wa 2021. Idadi ya watahiniwa ilikuwa kubwa sana. Ili kusaidia mchakato wa uteuzi wa wanajamii, zana ya ushauri wa upigaji kura itaundwa. Hii itakuwa sawa na zana ya ushauri wa upigaji kura iliyotumika kwa mchakato wa uteuzi wa Kamati ya Uandishi wa Hati ya Harakati.
Ratiba ya wakati
April 2022 |
|
Katikati ya Aprili - mapema Mei 2022 |
|
Mwishoni mwa Aprili - mapema Mei 2022 |
|
Katikati ya Mei - mapema Juni 2022 |
|
June 10, 2022 – June 17, 2022 |
|
June 18, 2022 – June 24, 2022 |
|
Late June |
|
June 24, 2022 – June 30, 2022 |
|
July 1, 2022 – July 15, 2022 |
|
Mid-July |
|
Katikati ya Julai - mapema Agosti 2022 |
|
Katikati ya Julai - katikati ya Agosti |
|
August 19, 2022 |
|
August 23, 2022 – September 6, 2022 |
|
September 6, 2022 – September 21, 2022 |
|
October 2022 |
|
Ushiriki wa shirika la ushirika
Mashirika washirika yatapiga kura katika uchaguzi huu Julai ili kuorodhesha wagombea sita kutoka kundi la wagombea. Kila shirika shirikishi litaruhusiwa kura moja. Kura hii itatumia mbinu ya Kura Moja Inayoamishika. Mashirika washirika yanapaswa kujadili wagombea ambao shirika washirika lingependa kuchagua. Wagombea wanapaswa kuorodheshwa kulingana na upendeleo.
The Affiliate Representatives were able to ask questions for the candidates to answer. Candidates published answers starting on June 24.
Ili kusaidia katika mchakato huu wa uteuzi, Kamati ya Uchambuzi itaundwa.
Kamati ya Uchambuzi
Kamati ya Uchambuzi inaundwa kutoka kwa washirika mwishoni mwa Aprili na Mei. Kamati ya Uchambuzi inaundwa na wawakilishi 9 wa washirika (pamoja na sura zote, vikundi vya watumiaji, na vikundi vya mada) kutoka kwa maeneo katika harakati. Kila moja kutoka:
- CEE (Ulaya ya Kati na Mashariki);
- ESEAP (Asia ya Mashariki na Kusini-mashariki, na eneo la Pasifiki);
- Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
- Amerika ya Kilatini na Visiwa vya Karibi;
- MENA (Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini);
- Amerika ya Kaskazini (Marekani na Kanada);
- Ulaya ya Kaskazini na Magharibi;
- Asia ya Kusini;
- Jumlisha moja kwa ajili ya washirika mada.
There was no representative from the Northern and Western Europe or South Asia.
Mchakato wa uteuzi wa kuunda Kamati ya Uchambuzi utabainishwa na washirika, kwa usaidizi wa Kamati ya Chaguzi na timu ya Mkakati na Utawala wa Harakati inapohitajika.
Kamati ya Uchambuzi hutathmini wagombea dhidi ya ujuzi na utofauti, usawa na vigezo vya ujumuishi vilivyoshirikiwa na Bodi ya Wadhamini. Kamati ya Uchambuzi itatumia taarifa ambazo wagombea hujibu kwenye maombi yao kuwakadiria wagombea. Kamati ya Uchambuzi itawatathmini wagombea kwa mfumo wa dhahabu/fedha/shaba. Ukadiriaji huu utatumika kutoa maoni kwa mashirika shirikishi yanapopanga kura yao. Maelezo ya tathmini ya kila mgombea hayatashirikiwa.
Baada ya wagombea sita kuchaguliwa wakati wa mchakato wa upigaji kura wa shirika shirikishi, ukadiriaji wa kila mgombeaji aliyechaguliwa utachapishwa ili kufahamisha kura ya jumuiya. Mchakato huu unalenga kupata uwiano bora kati ya kushirikisha taarifa muhimu na kupunguza udhihirisho usio wa lazima wa wagombea.
Wajumbe wa kamati waliochaguliwa
Process
The Analysis Committee worked from late May to mid-June. Details of their meetings and process can be found on the Analysis Committee Discussions.
The Board Selection Task Force and the Elections Committee developed a set of evaluation criteria for the Analysis Committee to evaluate candidates against. The Analysis Committee members assessed candidates individually. Only two Movement Strategy and Governance facilitators who supported the process had access to these individual scores.