Wikimedia Foundation Board of Trustees/Wito wa maoni: Chaguzi za Bodi ya Wadhamini
Timu ya Mkakati wa Harakati na Utawala ya Wikimedia Foundation inaunga mkono wito wa utoaji maoni kuhusu michakato ya uteuzi wa Bodi ya Wadhamini kuanzia tarehe 10 Januari hadi 16 Februari 2022. Utapata taarifa ya tatizo na angalau maswali mawili muhimu yatakayochunguzwa katika wito huu hapa chini. |
Tatizo la kutatua
Shirika la Wikimedia Foundation na harakati za Wikimedia vimekua zaidi kwa miaka kumi iliyopita, na Bodi kwa kiasi kikubwa imebaki ile ile katika muundo na mchakato.Katika ukaguzi wa utawala wa 2019, uwezo, utendakazi, na ukosefu wa uwakilishi wa watu wa aina mbalimbali katika harakati za Wikimedia vilionekana kuwa ni changamoto.
Mnamo 2021, baadhi ya hoja hizi zilijadiliwa wakati wa Wito wa Maoni: Viti vya Bodi ya Jumuiya. Uchaguzi wa 2021 wa Baraza la Wadhamini ulijumuisha mbinu zilizosasishwa ili kuanza kushughulikia masuala yaliyoorodheshwa hapo juu. Viti viwili vya ziada viliongezwa kushughulikia mahitaji ya uwezo wa Bodi. Upigaji kura mmoja unaoweza kuhamishwa ulitumiwa kuboresha fursa ya uwakilishi wa anuwai ya harakati. Wadhamini walishirikisha ujuzi wao na kuwataka wagombea kushirikisha ujuzi wao pia ili kuwafahamisha wapiga kura. Ufikiaji mpana na wa lugha nyingi ulisaidia kuwapata wagombea na wapiga kura kutoka katika jamii nyingi kwa kutumia njia nyingi za mawasiliano.
Katika wito huu wa utoaji maoni wa 2022 tunatumai kubainisha njia zaidi za kutatua changamotoili kuonyesha utofauti wa harakati kwenye Bodi. Zaidi ya hayo, tunataka kutumia fursa hii kujifunza kutoka kwa jamii kuhusu kushirikiana na wagombea wakati wa mchakato wa uchaguzi.
Muundo wa utoaji maoni
Kwa wito huu wa utoaji maoni, tunachukua mbinu tofauti inayojumuisha maoni ya jumuiya kutoka kwenye mchakato uliofanyika 2021. Badala ya kuongoza kwa mapendekezo, wito huo umeundwa kwa mfumo wa maswali muhimu. Nia ni kuhamasisha mazungumzo ya pamoja na juhudi za pamoja za kuboresha pendekezo la ushirikiano.
Asante kwa kuchukua muda kushiriki katika wito huu wa utoaji maoni na kusaidia kuunda Bodi ya Wadhamini yenye uwakilishi wa watu tofauti tofauti na inayofanya kazi vizuri.
Maswali muhimu
| ||
|
||
| ||
|
||
| ||
|
Jinsi ya kushiriki
Wafanyakazi wa Mkakati wa Harakati na Utawala wanaweza kusaidia mazungumzo katika lugha nyingi. Majadiliano yanakaribishwa katika lugha yoyote, ingawa tunaweza kuhitaji kutegemea watafsiri waliojitolea kusaidia kufanya muhtasari wa lugha ambazo hatuna wafanyakazi. Unaweza kupata viungo vya mazungumzo katika lugha nyingi kwenye jedwali kwenye ukurasa wa Maswali Muhimu. Unaweza kupata mazungumzo kwenye gumzo la uteuzi wa Bodi ya Telegramu. Wasiliana na mwezeshaji katika eneo lako ili kupanga mazungumzo ya jumuiya au kutoa maoni.
Rekodi ya matukio
- Tarehe 23 Desemba: Tangazo la Wito wa Maoni
- Tarehe 10 Januari: Wito wa utoaji wa Maoni utafunguliwa
- 16 Februari: Wito wa Maoni utafungwa
- 26 Februari: Kuchapisha ripoti ya mwisho ya Wito wa Maoni
Kila wiki timu ya Mkakati wa Harakati na Utawala utachapisha ripoti ya kila wiki ili kudaka maoni ya mrejesho na mjadala utakaokuwa umeendelea wiki iliyopita.
Taarifa muhimu ya utangulizi
Baraza la Wadhamini ndicho chombo cha utawala kinachosimamia Wikimedia Foundation, shirika la wafanyakazi 450+ linalosaidia harakati za kimataifa zinazoundwa na mamia ya miradi, jumuiya na washirika. Jukumu la pekee la Bodi ni kusimamia usimamizi wa utendaji wa Wikimedia. Hii ni pamoja na:
- Kushiriki katika kuweka mkakati wa muda mrefu wa Wakfu wa Wikimedia.
- Ufuatiliaji wa shughuli na fedha ili kuhakikisha kuwa fedha zipo za kutosha, zinalingana na dhamira na zinatii wajibu wa kisheria.
- Kuajiri, kusimamia, kushauri, na kuweka fidia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wikimedia Foundation.
Maelezo zaidi yanapatikana katika Kitabu cha Bodi.