Fundraising 2012/Translation/Isaac appeal/sw

This page is a translated version of the page Fundraising 2012/Translation/Isaac appeal and the translation is 100% complete.

 

  • Tafadhali soma:
    Mwito wa kibinafsi kutoka kwa
    Mhariri wa Wikipedia Isaac Kosgei

Appeal

Kutoka kwa mhariri wa Wikipedia Isaac Kosgei

Maarifa ni ya kila mtu, hata wale ambao hawana uelewa/uwezo wa kutumia mtandao wa intaneti. Siku hizi, shule nyingi nchini Kenya zina tarakilishi. Lakini nyingi bado hazina intaneti, sana sana maeneo ya vijijini katika nchi yangu.

Kama mhanga wa Wikipedia, mchango wangu mkuu ni usamabzaji wa toleo la Wikipedia lisilohitaji intaneti. Toleo hili ni la maandishi pekee.

Kusafiri kwa basi na teksi, huku tukiwa tumejiami kwa diski-ROM, diski-USB, kompyuta ya mkononi na projector, mie na rafiki zangu hutembelea mashule Kenya kote.

Sisi husakinisha Wikipedia katika makompyuta ya shule na kuwaelimisha walimu ambavyo mradi unavyoendeshwa. Kisha tunaipa shule mzima mifano tukitumia projector na kupeana hotuba ya umuhimu wa wikipedia

Walimu wanasema ya kwamba mradi huu umebadili maisha ya maelfu ya wanafunzi na unaleta mapinduzi katika elimu nchini kenya. Wanafunzi huwa wenye furaha na hutushukuru kwa vitendo hivi.

Kutokana na wikipedia - na safari kadha refu katika mabasi yaliyojawa na vumbi - kizazi kizima cha wanafunzi sasa kina kamusi elezo kubwa zaidi duniani. Ninavyoona, hili ndilo jambo bora zaidi kutendeka.

Unapochangia kwa Wikipedia, unabadilisha dunia. Kutoka kwa mvunguni mwa moyo wangu, asante.

Isaac Kosgei
Mwanafunzi wa Biashara na mhanga wa Wikipedia