MABADILIKO YA KIUFUNDI KWENYE SEVA
Hivi karibuni Wiki yenu itakuwa kwenye mfumo wa kutoharirika.
Soma ujumbe huu kupitia lugha nyingine • Please help translate to your language
Shirika la Wikimedia litafanya mbadilishano wa taarifa baina ya vituo vyake vya data. Hii itahakikisha kuwa Wikipedia na Wiki nyingine za Wikimedia zinabaki mtandaoni hata likitokea janga.
Mbadilishano wa taarifa utafanyika: 25 Septemba. Mbadilishano utaanza $muda huu:
Inasikitisha kwamba, kutokana na vipingamizi kwenye MediaWiki, uhariri wa kila namna itabidi usitishwe wakati wa mbadilishano. Tunaomba radhi kwa mvurugiko huo, na tunafanya juhudi kupunguza kutokea kwa adha kama hiyo siku za ver.
Bango litaanikizwa kwenye Wiki zote dakika 30 kabla ya kuanza kwa mchakato. Bango litabaki likionekana mpaka operesheni itapofikia mwisho.
Mtaweza kusoma, lakini si kuhariri, kwenye Wiki zote, kwa kipindi kifupi.
- Hutoweza kuhariri kwa takriban saa moja Jumatano 25 Septemba 2024.
- Ukijaribu kuhariri na kuhifadhi kwenye nyakati his, utaona ujumbe kukujulisha kuwa umekosea. Tunanatumaini kuwa hakuna maharirio yatakayopotea kwenye dakika hizo, lakini hatuwezi kuahidi. Ukiona ujumbe unaokuarifu kuwa unakosea, basi tafadhali subiri hadi iwe ya kawaida. Baadae utaweza kuhifadhi kuhifadhi maharirio yako. Kakini, tunashauri uweke kwanza nakala ya mabadiliko uliyofanya, kwa tahadhari tu.
Athari nyingine
- Shughuli za nyuma ya pazia zitakuwa za taratibu sana, na nyingine zinaweza kuachwa. Viungo vyekundu vinaweza vikasasishwa polepole kuliko kawaida. Ukianzisha makala makala ambayo tayari imeunganishwa na sehemu nyingine, kiungo kitabaki chekundu kwa muda mrefu kuliko kawaida. Baadhi ya maandishi ya muda mrefu italazimika kuyasimamisha.
- Tunatarajia utekelezaji wa kimsimbo utafanyika kama kwenye wiki [juma] zingine. Hata hivyo, kuzuiwa Kwa baadhi ya misimbo itayoainishwa, kunaweza kutokea bila kuchelewa kama operesheni itahitaji baadae.
- Gitlab haitopatikana kwa kiasi cha dakika 90.
Mradi huu unaweza kuahirishwa panapo ulazima. Unaweza kusoma ratiba hiyo kwenye wikitech. wikimedia.org. Mabadiliko yoyote yatatangazwa kwenye mpangilio wa ratiba.
Tafadhali shiriki habari hii na jumuia yako.