Wikimedia 2030
Mkakati wa wikimedia 2030 ninini?
Kwasasa, sisi nizaidi ya kundi la tovuti na miradi. Tumekua wanaharakati tulio jikita katika maadili na maono yenye tija. Sisi kwapamoja sasa tumepata fursa ya kujadili wapi tunaelekea kuanzia hapa. Tunaweza kujadili namna gani tunaweza kubali [maono] yetu kwenda kwenye uharisia. Tutakua tumefanikiwa nini kwa miaka kumi 10 kutoka sasa?
Tuko wapi kwa sasa?
Niwakati sasa wa kutengeneza mpango wa kuhakikisha mapendekezo ya harakatik mkakati yanaletwa kwenye uharisia, kwakupitia mtirirko wa matukio mpito. wanawikipedia wote wanakaribishwa katika matukio mubashara kuchukua nafasi ya kujadili pamoja mpango wa kuwezesha mapendekezo hayo yaweze kufanyiwa kazi.
Ninani anaeshughurikia Mkakati?
Harakati mkakati ya wikimedia 2030 umekua mchakato shirikishi na wa wazi.ikiwa umesimamiwa na wafanyakazi wa mradi wa wikimedia, mkakati umekua ukihusisha mfururizo wa ushauri wa kina kutoka kwa washiriki wa kujitolea. katika awamu yake ya kwanza, zaidi ya taarifa au kauli 1,800 kutoka jumuia au jamii miamoja zilijumuishwa kutengeneza mwelekeomkakati. Katika kipindi cha awamu ya pili, zaidi ya watu miamoja walijitolea kutoka katika jumuia na washiriki mbalimbali kutengeneza mapendekezo na kanuni, wakiwa wamearifiwa na maoni ya kina ya harakati.
Mwishoni mwa mwaka 2020, vikundi mbalimbali vya wanawikimedia kutoka katika jamii mbalimbali, kwakufuata mwongozo wa wiki-engagement and guidance, waliandaa mhtasari wa matukio mubashara ya mpito. Mchakato ulilenga zaidi juu ya uwazi na uhudhuriaji wa harakati ya kuijenga kesho yetu,zaidi kutoka katika miradi jamii na makundi mengine yaliyo kosa uwakirishi. Unakaribishwa kuungana kushiriki nasi katika matukio haya mubashara.