Maangazo ya Wikimedia, Agosti 2012

This page is a translated version of the page Wikimedia Highlights, August 2012 and the translation is 100% complete.



Maangazo kutoka kwa Ripoti ya Wakfu wa Wikimedia na Ripoti ya Uhasibu ya Wikimedia ya Agosti 2012, na chaguo ya matukio mengine ya maana kutoka kwa harakati ya Wikimedia

Maangazo ya Wakfu wa Wikimedia

 
Kielelezo-skrini cha programu tumizi ya Wiki Yapenda Minara (Wiki Loves Monuments)

Programu tumizi ya Wiki Yapenda Minara yawezesha michango ya watumizi wa kwanza wa simu ya rununu katika miradi ya Wikimedia

Kwa matayarisho ya "Wiki Yapenda Minara" ya Septemba, yale mashindano ya dunia nzima ya kuchanga picha za urithi wa utamaduni kwa Wikimedia commons, timu ya simu ya mkono ilitoa Programu tumizi mpya ya Wiki Yapenda Minara ya Android. Watumiaji wanaweza kutafuta minara ilyo karibu nao, ama watafute minara hiyo kutoka kwa orodha.Mtumiaji anaweza kuchukua picha kutoka ndani ya programu na moja kwa moja kuipakia kwa Wikimedia Commons. Hii ni mara ya kwanza utaratibu wa mchango kwa simu ya mkono unafanywa rasmi . Njia zingine za kuchangia miradi ya Wikimedia kutumia vifaa vya simu zinapojadiliwa pia.

Zana za kusaidia lugha zimetolewa katika "Project milkshake"

Timu ya Internationalisation/Localisation (i18n/l10n) iliripoti maendeleo katika Project Milkshake yake.Juhudi za kutolewa kwa viungo vya HatiJava vilivyofanywa kimataifa kama maktaba ya jQuery. Hii inajumuisha muundo mbinu wa i18n unaounga mkono kutua nafasi ya parameta na sarufi-, na tafsiri zilizo huru na jinsia, maktaba itakayounga mkono WeFonts. (fonti ambazo hazihitaji kusanikishwa katika kompyuta ya msomaji)

Ombi la maoni kwa programu ya ada ya fedha za kisheria

Katika Maombi ya Maoni, Wakfu unapendekeza programu inayopangiwa kusaidia kulipia ada ya kutetea kisheria watumijai katika majukumu fulani yaliyotajwa - Kwa mfano msimamizi fulani wa jamii, majibu ya barua pepe ama majukumu ya usimamizi wa miradi - kama kesi italetwa dhidi yao katika uhusiano na shughuli zao katika majukumu haya.

Mradi wa majaribio katika Wikipedia ya Kiarabu waongeza michango ya wahariri wapya

Katika Wikipedia ya Kiarabu, "Kituo kipya cha mchango" kilitengenezwa mnamo Juni kama mradi wa majaribio katika programu ya Programu ya Michango na Ukuaji wa wahariri. Ni hutoa mafunzo rahisi ya kuona kwa ajili ya kazi sita za msingi sitaza kuhariri, kama vile kukosoa makosa ya kosa la kuchapa au kujenga makala mapya.Imeongeza uwiano wa watumiaji wapya ambao huanza kuchangia, kulingana na uchambuzi wa awamu ya kwanza (katika Kiingereze na Kiarabu).

 
Kituo cha michango katika Wikipedia ya Kiarabu (awamu 0)

Takwimu na Mwelekeo

 
Mkutani wa vipimo vya Wakfu wa Wikimedia na shughuli, Septemba 4, 2012

Wageni wa kipekee wa Julai:

Milioni 451.82 (-3.82% ikilinganishwa na Juni , +14.81% ikilinganishwa na mwaka uliopita)

(Takwimu ya comScore ya miradi yote ya Wakfu wa Wikimedia; comScore itatoa takwimu za Agosti baadaye mnamo Septemba)

Maombi ya Kurasa ya Agosti:

bilioni 18.2 (+2.6 % ikilinganishwa na Juni; +20.7% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
(logi ya takwimu ya seva, Miradi yote ya Wikimedia ikijumuishwa na wanayoipata kwa njia ya simu)

Wahariri waliosajiriwa wa Julai 2012 (>=5 hariri/mwezi bila kujumuisha boti)

80,465 (+2.59% ikilinganishwa na Junii / +1.16% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
(Takwimu za hifadhidata, miradi yote ya wakfu wa Wikimedia. Ilani:Tumehamia kipimo bora ili kujumuisha Wikimedia commons na shughuli katika miradi yote.)

Kadi ya ripoti (kuunganisha data mbalimbali za takwimu na mwenendo kuhusu miradi WMF) ya Julai 2012:

http://reportcard.wmflabs.org/

(Fafanuzi)

Fedha

 
Wakfu wa Wikimedia mapato na matumizi mwaka hadi sasa ikilinganishwa na mpango mnamo Julai 31, 2012
 
Wakfu wa Wikimedia matumizi kwa majukumu mnamo Julai 31, 2012

(Habari ya kifedha inayopatikana ni ya Julai 2012 pekee wakati wa kuandika ripoti hii.)

Habari yote ya kifedha iliyowasilishwa ni ya Mwezi hadi sasa na Mwaka hadi sasa Julai 31, 2012.

Mapato $346,647
Matumizi:
 Kikundi cha uhandisi $1,145,753
 Kikundi cha Kuchangisha Fedha $221,223
 Kikundi cha maendeleo ya dunia nzima $541,308
 Kikundi cha usimamizi $96,465
 Sheria/Utetezi wa Jamii/Kikundi cha mawasiliano $185,852
 Fedha/HR/Kikundi cha usimamizi $413,077
Jumla ya Matumizi $2,603,678
Jumla ya mabaki/(hasara) ($2,257,031)
  • Mapato ya mwezi hadi sasa na ya mwaka hadi sasa ni dola elfu 347 ikilinganishwa na mpango wa dola milioni 1.5, kwa kukadiria ni $1.1 ama 76% chini ya mpango, kimsingi kwa sababu $1M kutoka kwa Wakfu wa Sloan ilibajetiwa kwa Julai lakini ikapokelewa Agosti.
  • Matumizi ya mwaka ya mwezi hadi sas na mwaka hadi sasa ni $2.6 ikilinganishwa na mpango $3.2M, kwa kukadiria $639K ama 20% chini ya mpango, kimsingi kwa sababu ya matumizi ya chini yanayohusisha wafanyikazi na zawadi na ruzuku zilizohusisha Wikimania DC ambayo ilikuwa imekadiriwa katika FY 11-12.
  • Msimamo wa kifedha ni dola milioni 23.6 mnamo Julai 31, 2012 ambayo kwa kukadiria ni matumizi ya miezi 6.7
Video ya mkutano wa kila mwezi wa vipimo vya Wakfu wa Wikimedia na shughuli ikiangazia mwezi wa Agosti (Sptemba 4, 2012)


 
Umbo la swara kutoka Mali (Moja ya picha zilizochangwa na "Raccolte Extraeuropee")

Maangazo mengine ya Harakati

Mchango wa picha za sanaa ya Kiafrika

Katika Wikimedia Commons, Mkusanyiko wa zanaa za Kiitaliano ("Raccolte Extraeuropee" Kutoka Milan) imekua ikipakia mamia ya picha ya kazi ya sanaa za Kiafrika, na maelezo ya undani. Katika Afrika yenyewe, (nyumba za sanaa,maktaba, nyaraka au vyumba vya makumbusho) zinaunga mkono mradi wa "WikiAfrica", wakati wengine wakishirikiana na Wikimedia Afrika Kusini na Wikimedia Kenya.

Wakutubi wa Kikatalani wapokea mafunzo ya Wikipedia

In a Mradi wa miezi miwili unaojumuisha mkusanyiko wote wa maktaba za umma za Kikatalani, wakutubu 150 walifunzwa jinsi ya kujuza watumizi wa maktaba zao kuhusu wikipedia. Ni ushirikiano wa kwanza kati ya Amical Viquipèdia na Wizara ya tamaduni ya Katalani. Wizara hiyo pia imechapa upya nakala 1,500 ya mwongozo wa "Karibu katika Wikipedia" ili usambazwa katika mtandao wa Maktaba.

Mkutano wa mwaka wa Lugha ya Kijerumani

WikiCon 2012, mkutano wa kila mwaka wa wana Wikimedia wanaoongea lugha zenye asili ya Kijerumani ulifanyika kwa muda wa siku tatu katika mji wa Dornbirn karibu na tripoint huko Austria, Ujerumani na Uswizi.Ulileta pamija washiriki zaidi ya 200 kutoka kwa miradi ya lugha za Kijerumani, majaribio mengine ya maarifa bure na raia wenye nia.Tukio hilo liliandaliwa na wahanga na ulifadhiliwa na sura za Wikimedia katika hizo nchi tatu, na Wakfu wa Wikimedia."Azimio la Dornbirn WikiCon 2012" ilipitishwa na katika mkutano huo.Miongoni mwa mada nyingine, nyaraka hiyo ilitoa wito kwa miongozo juu ya uhariri ya kulipwa, ushiriki zaidi wa wanawake, na sera rahisi kidogo za ufutaji wa faili za media ambazo hati miliki zao hazijulikani.