Wikimedia Foundation elections/2021/2021-08-18/2021 Voting Opens/sw

This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2021/2021-08-18/2021 Voting Opens and the translation is 100% complete.

Zoezi la upigaji kura la Uchaguzi wa Bodi ya wadhamini kwa 2021 sasa limefunguliwa. Wagombea kutoka jumuiya za Wikimedia waliombwa kuwasilisha maombi yao ya ugombea. Baada ya wito uliodumu kwa muda wa wiki tatu, kuna wagombea 19 kwenye uchaguzi huu wa mwaka 2021.

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation ndiyo inayoratibu shughuli zote za shirika hilo. Bodi inataka kuboresha weledi wake na utofauti wa wanabodi wake. Wameshirikisha maeneo ya ujuzi ambayo wanategemea yatafanyiwa kazi na hao wanabodi wapya watakaochaguliwa.

Harakati hizi zina nafasi ya kuchagua wagombea ambao wana ubora wa kukidhi mahitaji muhimu ya harakati hizi kwa miaka kadhaa ijayo. Muhula wa uongozi kwa hao watakaochaguliwa utaanza Septemba mwaka huu na kuisha baada ya miaka mitatu ijayo. Pata dondoo kidogo kuhusiana na Bodi ya Wadhamini kwenye hii video fupi.

Piga kura sasa mpaka Agosti 31.

Hapa chini kuna taarifa muhimu kuhusu harakati za uchaguzi.

Pata dondoo zaidi kuhusu wagombea

Wagombea kutoka jumuiya mbalimbali za Wikimedia wamewasilisha nia zao za ugombea. Pata dondoo kuhusiana kila mgombea ili ujue nani utampigia kura.Jumuiya ziliwasilisha maswali kwa kila mgombea ili yajibiwe na wagombea wakati wa kampeni. Wagombea walijibu orodha ya maswali yaliyoulizwa na wanajumuiya ambayo yamekusanywa na Kamati ya Uchaguzi katika Meta

Piga kura

Zoezi la upigaji kura kwa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini wa mwaka 2021 limefunguliwa mnamo 18 Agosti 2021 na litafungwa mnamo 31 Agosti 2021. Kamati ya Uchaguzi ilichagua mfumo wa kura moja inayoweza kupigwa kwa zaidi ya mara moja.Faida ya mfumo huu ni kwamba mpiga kura anaweza kupanga mapendekezo yake kutegemeana na kipaumbelea atakachoona kinafaa kuhusiana na wagombea hao. Pata dondoo zaidi kuhusu Vigezo vya kupiga kura, namna ya kupiga kura, na maswali yaulizwayo mara kwa mara kuhusu kupiga kura.

Tafadhali unaombwa kusaidia kuchagua watu watakao weza kukidhi mahitaji ya harakati kwa muda huu. Piga kura na usaidie kutangaza ili watu wengi zaidi wapige kura. Watakaochagulia watasaidia kuliongoza Shirika na kusaidia mahitaji ya harakati kwa miaka michache ijayo.

Wenu,

Kamati ya Uchaguzi