Wikimedia Foundation Board of Trustees/Call for feedback: Board of Trustees elections/Call for Feedback about the Board of Trustees elections is now open/Short/sw
Wito wa Maoni kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini umefunguliwa
Wito wa Maoni: Uchaguzi wa Baraza la Wadhamini sasa umefunguliwa na utafungwa tarehe 7 Februari 2022.
Kwa wito huu wa maoni, Timu ya Mkakati wa Harakati na Utawala inachukua mtazamo tofauti. Mtazamo huu unajumuisha maoni ya jumuiya kutoka 2021. Badala ya kuongoza kwa mapendekezo, wito huu unaundwa kulingana na maswali muhimu kutoka kwa Bodi ya Wadhamini. Maswali muhimu yalitoka kwenye maoni kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini wa 2021. Nia ni kuhamasisha mazungumzo ya pamoja na ukuzaji wa pendekezo shirikishi kuhusu maswali haya muhimu.
Katika ubora,
Mkakati wa Harakati na Utawala