Fundraising 2012/Translation/Launch email
- NOTE TO TRANSLATORS
This letter is a new translation request, but re-uses large parts of the 2012 Jimmy Appeal.
If the 2012 Jimmy Letter has been translated into your language, you can probably re-use much of it for this translation. :-)
Pages for translation: [edit status] | |
Jimmy Appeal (source) |
Ready |
Landing Page and Banner messages (source) |
Ready |
Donor information pages (source) All languages | Missing - Please Translate |
Launch email (millions)
Salaam firstname,
Mchango wako uliendeleza Wikipedia mwaka 2012, tafadhali saidia kuiendeleza mwaka ujao kwa kutoa mchango wako leo.
Mchango mdogo unafanya kazi nyingi hapa Wikipedia. Pengine Google ina mashine za seva karibu milioni 1, Yahoo wana wafanyakazi 12,000. Sisi katika Wikipedia tuna seva 800 na wafanyakazi 150. Usimamizi wa mitambo unaendeshwa na watu wachache sana. Ofisi ya Wikipedia haikuweza kunenepa – wanenepe wengine!
Wikipedia ni tovuti ya tano duniani kwa hesabu ya kutembelewa. Kila mwezi watu milioni 450 hutembelea tovuti yetu – wakiangalia mabilioni ya kurasa zetu.
Si vibaya kufanya biashara au kuonyesha matangazo ya kibiashara – lakini hapa si mahala pake. Siyo katika Wikipedia.
Wikipedia ni kitu maalumu. Ipo kama maktaba au mahali pa umma. Pako kama hekalu la maarifa. Ni mahali ambapo wote twaweza kwenda na kutafakari, kujifunza, na kuwagana maarifa yetu na wengine.
Nilipoanzisha Wikipedia ingekuwa rahisi kuijenga kama biashara na tovuti inayozalisha pesa nyingi kwa njia ya kuonyesha matangazo ya kibiashara. Lakini sikutaka. Kwa hiyo tumejenga Wikipedia kwa pesa kidogo hasa kwa kujitolea na zawadi za wachangiaji.
Kama kila msomaji wa barua pepe hii angetoa kiasi kilekile aliyetoa mwishoni tusingehitaji kuomba kitu. Lakini si wote wanaoweza au wanaotaka kujitolea kwa njia hii. Hata hivyo tumepata wasaidizi wa kutosha hadi sasa.
Ninakuomba: usaidie mwaka huu tena. Ujitolee kwa dola 5, 10, 100 au jinsi unavyoweza. Tuendelee kujenga Wikipedia.
Ahsante,
Jimmy Wales
Mwanzilishi wa Wikipedia
Launch email (thousands)
Salaam $firstname,
Mchango wako uliendeleza Wikipedia mwaka 2012, tafadhali saidia kuiendeleza mwaka ujao kwa kutoa mchango wako leo.
Mchango mdogo unafanya kazi nyingi hapa Wikipedia. Google na Yahoo zina maelfu ya seva na wafanyakazi. Sisi tuna seva kama 800 na wafanyakazi kama 150. Usimamizi wa mitambo unaendeshwa na watu wachache sana. Ofisi ya Wikipedia haikuweza kunenepa – wanenepe wengine!
Wikipedia ni tovuti ya tano duniani kwa hesabu ya kutembelewa. Kila mwezi watu milioni 450 hutembelea tovuti yetu – wakiangalia mabilioni ya kurasa zetu.
Si vibaya kufanya biashara au kuonyesha matangazo ya kibiashara – lakini hapa si mahala pake. Siyo katika Wikipedia.
Wikipedia ni kitu maalumu. Ipo kama maktaba au mahali pa umma. Pako kama hekalu la maarifa. Ni mahali ambapo wote twaweza kwenda na kutafakari, kujifunza, na kuwagana maarifa yetu na wengine.
Nilipoanzisha Wikipedia ingekuwa rahisi kuijenga kama biashara na tovuti inayozalisha pesa nyingi kwa njia ya kuonyesha matangazo ya kibiashara. Lakini sikutaka. Kwa hiyo tumejenga Wikipedia kwa pesa kidogo hasa kwa kujitolea na zawadi za wachangiaji.
Kama kila msomaji wa barua pepe hii angetoa kiasi kilekile aliyetoa mwishoni tusingehitaji kuomba kitu. Lakini si wote wanaoweza au wanaotaka kujitolea kwa njia hii. Hata hivyo tumepata wasaidizi wa kutosha hadi sasa.
Ninakuomba: usaidie mwaka huu tena. [$1 Ujitolee kwa dola 5, 10, 100] au jinsi unavyoweza. Tuendelee kujenga Wikipedia.
Ahsante,
Jimmy Wales
Mwanzilishi wa Wikipedia