Mpango wa Mwaka wa Shirika la Wikimedia Foundation/2024-2025/Malengo
Shirika la Wikimedia Foundation lina malengo makuu manne mwaka wa 2024-2025. Yameundwa ili kuwiana na Mwelekeo wa KImkakati wa Harakati za Wikimedia na Mapendekezo ya Mkakati wa Harakati, na kuendeleza zaidi kazi iliyoainishwa katika mpango wa mwaka jana. Ambazo ni:
- MIUNDOMBINU: Kukuza Maarifa kama Huduma. Kuboresha Uzoefu wa Mtumiaji kwenye wiki, hasa kwa wahariri mahiri.Kuimarisha vipimo na kuripoti.
- USAWA: kusaidia Usawa wa Maarifa. Kuimarisha Usawa katika Kufanya Maamuzi ndani ya Harakati, kuendeleza usambazaji wa rasilimali kwa usawa, kusaidia jumuiya ili kuziba mapengo ya maarifa, na kukuza usawa duniani kote na uhusiano wa kikanda.
- USALAMA & UADILIFU: Kulinda watu na miradi yetu. Kuimarisha mifumo inayotoa usalama kwa wanaojitolea. Kutetea uadilifu wa miradi yetu. Kuendeleza mazingira ya maarifa ya bure kwenye miradi ya Wikimedia. (Kumbuka: hili limebadilishwa jina kutoka kuwa lengo la Usalama na Ushirikishwaji ikilinganishwa na mwaka jana.)
- UFANISI: Kuimarisha utendakazi wetu kwa ujumla. Kutathmini, Kurudia, na Kukabiliana mchakato wetu ili kupata matokeo ya juu zaidi kwa kutumia rasilimali chache zaidi.
Miundombinu |
Usawa |
Usalama na Uadilifu |
Ufanisi |
Vipimo: Kupima maendeleo kuelekea malengo yetu
Ili kupima maendeleo kuelekea malengo yetu, tumetambua seti ndogo ya vipimo vya msingi ambavyo Shirika la Wikimedia Foundation linapanga kuleta tija kupitia hivyo kwa mwaka ujao. Vipimo hivi vinafaa kuhamasisha kazi yetu na kutumika kama ishara kuashiria kama sisi wanasonga katika mwelekeo sahihi. Ambapo hatuoni athari tunayotarajia, tutarekebisha kazi yetu ili kupata matokeo tunayohitaji.
Vipimo vya msingi vilichaguliwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo:
- Tunaamini kuwa kipimo kinaonyesha kuwa tunasonga katika mwelekeo sahihi kuelekea malengo yetu.
- Tunaamini kuwa tunaweza kupima maendeleo yetu kuelekea kukiletea tija kipimo katika kipindi cha mwaka wa fedha.
- Tunaweza kupima mabadiliko katika kipimo kila baada ya miezi mitatu ili tuweze kusahihisha kama inavyohitajika katika mwaka mzima wa fedha.
- Tuna uwezo wa kupima na kuweka msingi kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha.
Matokeo ya kazi yetu yenye athari kubwa yanahitaji muda ili tija kuonekana. Kwa sababu hii, tutafuatilia maendeleo yetu kwa kutumia viashirio vikuu na hatua muhimu zinazohusiana na kila moja ya vipimo vya msingi. Kwa kuongeza, kuna pointi za ziada za data ambazo Shirika litafuatilia katika mwaka ujao kwa mtazamo kamili zaidi.
Shirika la Wikimedia Foundation limebainisha maeneo makuu manne ya kipimo cha 2024−2025.
- MAUDHUI: Kuongeza ubora na uaminifu wa maudhui ya kiinsaiklopedia.
- WACHANGIAJI: Kudumisha na kuboresha afya ya jumuiya za wachangiaji wa Harakati.
- UMUHIMU: Kuhakikisha umuhimu na uendelevu wetu kwa hadhira pana duniani kote.
- UFANISI: Kuhakikisha uendelevu wetu wa muda mrefu kwa kuboresha jinsi Shirika linavyofanya kazi na kukua.
Maudhui: Kuongeza ubora na uaminifu wa maudhui ya kiensaiklopedia
Dhamira yetu ni kuhakikisha kuenea kwa maarifa bila malipo duniani kote, na yaliyomo kwenye miradi yetu ni njia kuu ya kutoa ufikiaji wa maarifa bila malipo. Harakati zetu zimekuwa na matokeo ya mazuri kwa kiwango kikubwa na jumuiya zetu zimetumia miaka mingi kuboresha yaliyomo kwenye miradi yetu. Kupitia majaribio na ushirikiano, tumepata njia za manufaa za kuunga mkono juhudi zinazoendelea za jumuiya zetu ili kuongeza maudhui bora na ya kuaminika. Lugha, maeneo na mada maeneo ambapo tunaweza kuwa na tija ni pale ambapo pia tunaboresha usawa wa maarifa bila malipo duniani kote. Kwa kuzingatia kupanda kwa maudhui yaliyozalishwa na AI hivi majuzi, thamani ya maarifa yaliyoundwa na binadamu huongezeka mara nyingi. Ufanisi wa mbinu zinazotumiwa kuongeza ukuaji wa maudhui yanayoaminika ni viashirio vya maendeleo mazuri ambayo jumuiya zetu zinaweza kutegemea. Lengo letu mwaka huu wa fedha ni kutoa zana na mifumo inayosaidia uwezo wa wachangiaji kutambua na kuziba mapungufu ya maarifa.
- Lengo: Metriki hii inaelekeza kwenye lengo letu la kiwango cha juu la Usawa.
- Kipimo: Tutaongeza idadi ya makala bora kwenye Wikipedia. We will measure our success this year based on achieving the key results outlined under the Equity goal: Closing Knowledge Gaps.
Wachangiaji: Kudumisha na kuboresha afya ya jumuiya za wachangiaji wa Harakati
Mafanikio ya Wikipedia na kufikia kimataifa inategemea uendelevu wa jumuiya zetu za kujitolea, ambao hufanya kazi ya kujenga na kulinda miradi. Tunajua kutokana na kuzungumza na wafanyakazi wa kujitolea, kutoka kwenye data na utafiti, na kutoka kwenye ulimwengu wa nje kwamba uendelevu wa jumuiya zetu uko hatarini. Shirika husaidia kuhakikisha mafanikio na afya ya jumuiya zetu kwa njia nyingi: kwa kuboresha zana kwa wahariri wenye uzoefu, kujenga njia kwa wageni kuchangia kwa haraka na kwa ufanisi, kukuza uhusiano wa kikanda na kimataifa, kufanya kazi ili kulinda wafanyakazi wa kujitolea ambao usalama wao unatishiwa, kuunga mkono utawala wa kujitolea, na kutoa ruzuku kwa washirika wa harakati.
Tunalenga kukuza vizazi vingi vya watu wa kujitolea na kujenga jumuiya zinazostawi za kujitolea. Kwa sababu jumuiya zetu ni tofauti na zina majukumu mengi tofauti ya wachangiaji (watendaji, waandaaji, wahariri wa maudhui, watu wapya, n.k), tutatumia hatua za ziada zinazohusiana na kipimo chetu cha msingi kutathmini maendeleo yetu. Hatua hizi hujengwa kutokana na data ya michango katika miradi yetu, tafiti za maoni ya jamii na vipimo vya matokeo ya programu.
- Malengo: Kipimo hiki kinaonyesha malengo yetu ya kiwango cha juu ya Miundombinu, Usawa, na Usalama & Uadilifu.
- Measurement: We will measure our success this year based on achieving the key results outlined under Infrastructure, Equity, and Safety & Integrity. We will monitor the impact of our work across multiple points in the contributor journey, from newcomers to experienced editors, administrators, and moderators.
Umuhimu: Kuhakikisha umuhimu na uendelevu wetu kwa hadhira pana duniani kote
Wikipedia ni nyenzo ya ulimwengu kupata, kujifunza, na kushirikisha maarifa bila malipo. Kwa sehemu tunahukumu mafanikio ya kazi yetu kulingana na usomaji wetu, utumiaji tena wa maudhui yaliyoidhinishwa bila malipo, na uwezo wetu wa kuchangisha fedha ili kuendeleza malengo mapana ya Harakati yetu. Harakati ya maarifa ya bure inakabiliwa na changamoto nyingi. Wanaotafuta maarifa wanageukia fomu fupi, maudhui yanayotokana na utu. Utafutaji unabadilika kutokana na kuongezeka kwa Akili Bandia (AI). Mitandao ya kijamii hutumia video, sauti, na Kujifuna kwa Mashine(ML) zinayoendeshwa kwa algorithm ya mapendekezo badala ya maandishi na wavuti wazi ili kushirikisha hadhira. Kukabiliana na changamoto hizi kunahitaji mawazo mapya kuhusu nyanja nyingi - kuchangisha pesa, kutafuta watazamaji wapya, na kujihusisha kwa ubunifu na ulimwengu unaobadilika.
- Malengo: Metriki hii inaelekeza kwa lengo letu la kiwango cha juu la Miundombinu.
- Kipimo: Tutaongeza idadi ya vifaa vya kipekee kwenye Wikipedia. We will measure our success this year based on achieving the key results outlined under Infrastructure.
Ufanisi: Kuhakikisha uendelevu wetu wa muda mrefu kwa kuboresha jinsi Shirika linavyofanya kazi na kukua
Tumechagua uwiano wa gharama za kiprogramu kama kipimo chetu cha ufanisi wa Shirika. Uwiano wa gharama za kiprogramu ni kipimo cha kiasi cha fedha kinachoenda kwa programu dhidi ya gharama za usimamizi. Ni kipimo kinachotumika na kilichobainishwa vyema cha uwajibikaji wa kifedha kinachotumiwa na huduma kama vile Charity Navigator ili kutathmini ufanisi wa mashirika yasiyo ya faida. Hatua hii inatokana na maelezo yanayopatikana kwa umma kutoka kwenye Fomu yetu 990 kwenda kwenye IRS.
Hatua hii ya ufanisi huanzisha njia kwa Shirika kutathmini ubadilishanaji wa rasilimali muhimu na athari zake. Inatusaidia katika kuwasilisha biashara hizi kwa wadau wetu. Pia hutusaidia kuhakikisha kwamba tunatenga sehemu kubwa zaidi ya bajeti yetu kwa shughuli zinazosaidia moja kwa moja dhamira yetu kulingana na au kuzidi mbinu bora za sekta isiyo ya faida.
- Malengo: Metriki hii inaoana na lengo letu la kiwango cha juu la Ufanisi.
- Kipimo: Tutadumisha uwiano wetu wa gharama za kiprogramu kwa 77%.