Chaguzi za shirika la Wikimedia/2022/Miongozo ya ustahiki wa mpigakura

This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2024/Voter eligibility guidelines and the translation is 100% complete.

Wahariri

unaweza kupiga kutoka kwa jina moja tuu la mtumiaji lililo sajiliwa. Unaweza kupiga kura mara moja tu, Bila kujali una akaunti ngapi katika miradi ya Wikimedia. Ili uweze kuwa na sifa za kupiga kura unatakiwa kuwa na:

  • Usiwe umezuiliwa zaidi ya mradi mmoja;
  • na usiwe bot;
  • na uwe umefanya angalau mabadiliko 300 kabla ya tarehe 4 Agosti 2024 kwenye Wikimedia;
  • na uwe umefanya angalau mabadiliko 20 kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024.

Zana ya Ustahiki wa Akaunti inaweza kutumiwa ili kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Wasanidi-programu

Wasanidi programu wana sifa za kupiga kura ikiwa:

  • ni wasimamizi wa seva za Wikimedia walio na ufikiaji wa nje
  • au wameweka angalau ahadi moja iliyounganishwa kwa Wikimedia repos kwenye Gerrit, kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024

Kigezo cha ziada

  • au umeweka angalau ahadi moja iliyounganishwa kwa repo yoyote katika nonwmf-extensions au nonwmf-skins , kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024.
  • au wameweka angalau ahadi moja iliyounganishwa kwa repo yoyote ya zana ya Wikimedia (kwa mfano magnustools) kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024.
  • au watunzaji/wachangiaji wa zana, roboti, vifaa na moduli zozote za Lua kwenye Wikimedia wiki.
  • au wamejihusisha kwa kiasi kikubwa katika kubuni na/au kukagua michakato ya maendeleo ya kiufundi inayohusiana na Wikimedia.

Watafsiri

Watafsiri watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wamefanya angalau mabadiliko 300 kabla ya tarehe 4 Agosti 2024, na mabadiliko 20 kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024, kwenye translatewiki.net.

Wafanyakazi na wakandarasi wa Wikimedia Foundation

Wafanyakazi wa sasa wa Wikimedia Foundation na wanakandarasi watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wameajiriwa na Shirika kufikia tarehe 4 Agosti 2024.

Wafanyakazi na wakandarasi wa washirika wa Wikimedia

  • Ukurasa wa sasa wa Wikimedia, shirika la mada au wafanyakazi wa kikundi cha watumiaji na wanakandarasi wanahitimu kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kuanzia 4 Agosti 2024.
  • Wanachama wa mashirika rasmi kama ilivyofafanuliwa katika sheria ndogo za Sura za sasa za Wikimedia, mashirika ya mada au vikundi vya watumiaji wanahitimu kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika utendaji huo kuanzia 4 Agosti 2024.

Kamati ya Ushirikiano na Kamati ya Uchaguzi itathibitisha orodha ya Washirika wa Wikimedia wanaoruhusiwa kufikia tarehe 1 Agosti 2022.

Wajumbe wa bodi ya Shirika la Wikimedia na wajumbe wa bodi ya Ushauri

Washiriki wa sasa na wa zamani wa Bodi ya Usimamizi ya Shirika la Wikimedia na Bodi ya Ushauri ya Shirika Wikimedia wanastahili kupiga kura.

Wanachama wa kamati za harakati za Wikimedia

Wanachama wa sasa wa kamati za harakati za Wikimedia wanastahiki kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo kuanzia tarehe 4 Agosti 2024.

Kwa madhumuni ya mwongozo huu, kamati za harakati za Wikimedia zinafafanuliwa kama Kamati ya Mawasiliano, Kamati ya Uchaguzi, Kamati za Kuandaa Hati ya Harakati, Kamati kwa Lugha, na Kamati ya Uhariri ya Kanuni ya Maadili ya Ulimwenguni.

Waandaaji wa jumuiya ya harakati za Wikimedia

Watengenezaji wa jumuiya wenye sifa nzuri, ambao hawawezi kupiga kura katika makundi mengine, wana haki ya kupiga kura ikiwa wanatimiza mojawapo ya yafuatayo:

  • wametuma maombi, kupokea na kuripoti angalau ruzuku moja ya Wikimedia Foundation tangu 4 Agosti 2024.
  • walikuwa waratibu wa angalau tukio moja la hackathon lililofadhiliwa, shindano au tukio lingine la Wikimedia lililo na hati za Wiki na angalau wahudhuriaji/wageni/washiriki 10 kati ya 6 Septemba 2022 na 4 Agosti 2024.

Zingatia

Ikiwa unakidhi vigezo vikuu, utaweza kupiga kura mara moja. Kwa sababu za kiufundi zaa SecurePoll, watu wanaotimiza vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa watimize vigezo vingine. Iwapo unaona kuwa umekidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa board-elections@lists.wikimedia.org ukitumia hoja angalau siku nne (4) kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, mnamo au kabla ya 13 Septemba 2024. Ikiwa unakidhi vigezo, tutakuongeza kwenye orodha ya mwongozo, ili uweze kupiga kura.