Kamati ya Masuala ya Jamii ya Mradi wa Wikimedia/Utaratibu wa Maisha miradi Ndugu/Mwaliko wa kutoa mrejesho (MM)

Maoni ya mrejesho yamekaribishwa kwaajili hatua ya maisha mzunguko ya miradi ndugu

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language
 

Wapendwa wanajemii,

Kamati ya Masuala ya Jumuiya (CAC) ya Wikimedia Foundation Board of Trustees inakualika utoe maoni kuhusu rasimu ya Utaratibu wa Maisha ya Miradi Ndugu '. Rasimu hii ya Utaratibu inaeleza hatua zilizopendekezwa na mahitaji ya kufungua na kufunga Miradi Ndugu ya Wikimedia, na inalenga kuhakikisha kuwa miradi mipya iliyoidhinishwa inaanzishwa kwa mafanikio. Hii ni tofauti na taratibu za kufungua au kufunga matoleo ya lugha ya miradi, ambayo yanashughulikiwa na Kamati ya Lugha au sera ya kufunga miradi.

Unaweza kupata maelezo kwenye ukurasa huu, pamoja na njia za kutoa maoni yako kuanzia leo hadi mwisho wa siku mnamo Juni 23, 2024, popote pale Duniani.

Unaweza pia kutoa taarifa au maelezo kuhusu hili kwakushirikiana na jumuiya zinazovutiwa na miradi unaofanya nao kazi au kuunga mkono, na unaweza pia kutusaidia kutafsiri hatua au taratibu katika lugha nyingine zaidi, ili watu wajiunge na majadiliano katika lugha yao wenyewe.

Kwa niaba ya CAC,