Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Miongozo ya utekelezaji iliyorekebishwa/taarifa ya Wapigakura

This page is a translated version of the page Universal Code of Conduct/Revised enforcement guidelines/Voter information and the translation is 94% complete.
Outdated translations are marked like this.
Universal Code of Conduct

Upigaji kura wa kuidhinisha rasmi Miongozo ya Utekelezaji ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (UCoC) umepangwa kufanyika tarehe 17 Januari 2023 hadi 31 Machi 2023 kupitia SecurePoll. Wapigaji kura wote wanaostahiki miongoni mwa Jamii ya Wikimedia watakuwa na fursa ya kuunga mkono au kupinga matumizi ya Miongozo ya Utekelezaji, na kutoa sababu. Uidhinishaji rasmi wa miongozo ya utekelezaji ni muhimu ili kuweka mbinu na michakato ya utekelezaji wa UCoC. Hapa chini kuna maelezo zaidi kuhusu maagizo ya kupiga kura na ustahiki wa mpigaji kura.

Pia tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Upigaji Kura kwa maelezo kuhusu kupiga kura.

Mchakato wa kupiga kura

Ikiwa unastahiki kupiga kura:

 1. Pitia miongozo ya utekelezaji iliyorekebishwa ili kuona sera ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili.
 2. Amua kuungama au kupinga matumizi ya Miongozo ya Utekelezaji. Ikiwa unapinga miongozo hii, andika mapendekezo yako ya mabadiliko kwenye Miongozo ili kujumuisha pamoja na kura yako.
 3. Jifunze jinsi ya kurekodi kura yako ukitumia SecurePoll.
 4. Nenda kwenye ukurasa wa Upigaji Kura wa SecurePoll na ufuate maagizo.
 5. Kumbusha wanajamii wengine kupiga kura!

Ni nini kinachopigiwa kura?

Katikati ya Januari, Miongozo ya Utekelezaji (EGs) kwa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili itapigiwa kura ya pili ya uidhinishaji wa jamii nzima. Hii inafuatia kura ya Machi 2022, ambayo ilitoa matokeo ya watu wengi walioungwa mkono, lakini ikaangazia masuala muhimu ya jamii ambayo Kamati ya Bodi ya Masuala ya Jamii (CAC) iliomba kufanyiwa marekebisho. Kamati ya Marekebisho ilipitia maoni ya jamii na kufanya mabadiliko. Maeneo husika, kama vile kusawazisha faragha na uwazi, pamoja na mahitaji ya mafunzo na uthibitisho, yamesasishwa.

Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation inaunga mkono kura ya jamii kuhusu pendekezo la miongozo ya utekelezaji ya UCoC kufuatia uidhinishaji rasmi wa UCoC na Bodi yenyewe. Wadhamini pia wanatambua kuungama kura hiyo kwa barua ya pamoja ya Kamati za Usuluhishaji na utafiti wa maafisa wajitoleaji, wanachama washirika, na kamati ya kutengeneza rasimu.

Mojawapo ya mapendekezo makuu ya malengo ya kimkakati ya mwaka 2030 ilikuwa utengenezaji wa UCoC ili iwe msingi wa kote ulimwenguni wa tabia zinazoruhusiwa kwa mradi bila kuruhusu unyanyasaji.

Miongozo ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili

Miongozo hii ni ya utekelezaji Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Hapo awali UCoC iliidhinishwa rasmi na Bodi ya Wadhamini, ingawa bado haijaidhinishwa na jamii. Inajumuisha hatua za uzuiliaji, ugunduaji, na uchunguzaji na hatua nyingine zinazochukuliwa ili kukabiliana na ukiukaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Kimsingi, utekelezaji unashugulikiwa na, lakini sio tu, maafisa wateule kote kwenye miradi, matukio, na maeneo husika kwenye majukwaa ya wahusika wengine wa Wikimedia ya mtandaoni au nje ya mtandao. Itafanywa kwa mpangilio mzuri wa kimuda na kwa usawa Katika haraati mzima za Wikimedia.

Miongozo ya Utekelezaji UCoC ina sehemu mbili:

 • Kazi za uzuiliaji
  • Kukuza ufahamu wa UCoC, kupendekeza mafunzo wa UCoC, miongoni mwa mengine.
 • Kazi za uitikiaji
  • Kutoa maelezo ya mchakato wa kuwasilisha faili, kuchakata ukiukaji ulioripotiwa, kutoa nyenzo kwa ukiukaji ulioripotiwa, kuainisha hatua za utekelezaji kwa ukiukaji, n.k.

Kwa nini unapaswa kupiga kura?

Uidhinishaji rasmi wa miongozo ya utekelezaji ni muhimu ili kufanikisha mbinu na michakato na hata za utekelezaji wa UCoC. Upigaji kura kuhusu Miongozo ya Utekelezaji umebuniwa ili kutathmini jinsi jamii inaungama UCoC na ili kukusanya maoni kama wapigaji kura wana wasiwasi kuhusu mapendekezo ya sasa. Ni muhimu kuhakikisha sauti yako inasikika kupitia kura yako na ikiwa unachagua "hapana", ni muhimu kubainisha ni sehemu gani ya miongozo ambayo unawasiwasi nayo, na kwa nini.

Muhimu zaidi, upigaji kura utaweza:

 • Hakikisha kuwa maoni ya mradi wako wa Wikimedia yanawakilishwa katika kura ya kimataifa.

Jinsa ya kupiga kura

 
Muhtasari wa kura ya SecurePoll. Kumbuka haswa kwamba votewiki inaweza kupendekeza kuwa hujaingia. Kura yako bado itahesabiwa.

Tafadhali soma sehemu hii kabla ya kwenda kwenye SecurePoll ili kupata maelezo muhimu ili kurahisisha mchakato wako wa kupiga kura.

 • Kura itatoa swali la kupiga kura na kutoa chaguzi mbili. Tafadhali chagua "hapana" au "ndiyo". Kura zisizo na "hapana" au "ndiyo" zilizochaguliwa hazitajumuishwa katika hesabu ya mwisho.
 • Kisanduku cha "Maoni" kitakupa nafasi ya wewe kuacha maoni kuhusu masuala yoyote uliyo nayo kuhusu miongozo inayopendekezwa.
 • Kisha SecurePoll itakuarifu kwamba kura yako imerekodiwa.
 • Unaweza kupiga kura tena katika uchaguzi. Inafuta na kurekodi upya kura yako. Unaweza kufanya hivyo mara nyingi kadri utakavyo.

Matokeo ya kura yatabainishwa vipi?

Kiwango cha juu cha usaidizi cha zaidi ya 50% cha watumiaji wanaoshiriki kitahitajika ili kuhamia kwenye uidhinishaji wa Bodi ya Wadhamini. Kwa sasa, harakati hazina mbinu moja ya kufuata ya kubaini mchakato wa kupiga kura uliofaulu/kutofaulu (baadhi ya mbinu hutumia mbinu ya kura nyingi kwa njia kubwa (⅔), huku mbinu nyingine zikitumia wingi wa kura tu (50% +1), ilhali mbinu nyingine zinaepuka kuhesabu idadi ya kura). Kwa mchakato huu, ili kuendanisha na kura nyingi za maoni katika mamlaka nyingi ulimwenguni, mbinu ya wingi wa kura ilichaguliwa.

Kura zitachunguzwa na kundi huru la watu waliojitolea, na matokeo yatachapishwa. Kama ilivyo kwa kura ya kwanza, wapiga kura wataweza kupiga kura na kutoa hoja walio nazo kuhusu miongozo. Bodi ya Wadhamini itaangalia viwango vya usaidizi na hoja zinazotolewa wanapoangalia jinsi Miongozo ya Utekelezaji inapaswa kuidhinishwa au kuendelezwa zaidi.

Watu wa nje ya Wikimedia Foundation watahusika katika kufuatilia upigaji kura ili kuhakiki uhalali?

Matokeo ya kura yatachunguzwa kwa dosari na Wanawikimedia wa kujitolea walio na uzoefu Katika upigaji kura wa harakati na michakato ya uthibitishaji. Wachunguzi wa kura watatangazwa baadaye.

Ustahiki wa kupiga kura

Kanuni ya jumla

Hupaswi kuzuiwa katika zaidi ya mradi mmoja ili uhitimu kupiga kura.

Wahariri

Unaweza kupiga kura kutoka kwa akaunti yoyote moja iliyosajiliwa unayomiliki kwenye tovuti ya Wikimedia. Unaweza tu kupiga kura mara moja, bila kujali ni akaunti ngapi unazomiliki. Ili kuhitimu, akaunti hii lazima:

 • isizuiliwe kutoka kwa zaidi ya mradi mmoja;
 • na isiwe roboti;
 • na iwe imefanya angalau maharirio 300 kabla ya tarehe 7 Januari 2023 katika tovuti zote za Wikimedia;
 • na iwe imefanya angalau maharirio 20 kati ya tarehe 3 Julai 2022 na 3 Januari 2023.

Zana ya Ustahiki wa Akaunti inaweza kutumiwa ili kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Watengenezaji

Watengenezaji wanahitimu kupiga kura ikiwa:

 • ni wasimamizi wa seva ya Wikimedia wenye ufikiaji wa Shell
 • au ametoa angalau mchango mmoja kwa Wikimedia repos kwenye Gerrit, kati ya tarehe 3 Julai 2022 na 3 Januari 2023.

Vigezo vya ziada

 • au amefanya angalau mchango mmoja kwenye akiba yoyote Katika nonwmf-extensions au nonwmf-skins, kati ya tarehe 3 Julai 2022 na 3 Januari 2023
 • au amefanya angalau mchango mmoja kwenye akiba yoyote ya zana ya Wikimedia (kwa mfano [1]) kati ya tarehe 3 Julai 2022 na 3 Januari 2022
 • au amefanya angalau maharirio 300 kabla ya tarehe 7 Februari 2022 na amefanya angalau maharirio 20 kati ya tarehe 3 Julai 2022 na 3 Januari 2023 kwenye translatewiki.net.
 • au wadumishaji/wachangiaji wa zana, roboti, programu za watumiaji, vifaa, na moduli zozote za Lua kwenye tovuti za Wikimedia;
 • au wamehusika pakubwa katika michakato ya kubuni na/au kuhakiki utengenezaji wa kiufundi unahusiana na Wikimedia.

Kumbuka: Ikiwa unakidhi vigezo kuu, utaweza kupiga kura mara moja. Kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi vya SecurePoll, watu wanaotimiza vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa watimize vigezo vingine. Kama unafikiri umekidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa ucocproject@wikimedia.org pamoja na hoja hizo angalau siku nne kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, tarehe 27 Januari 2023 au kabla. Ukitimiza vigezo, tutakuongeza kwenye orodha ya mwongozo, uweze kupiga kura.

Wafanyikazi na wakandarasi wa Wikimedia Foundation

Wafanyikazi na makontrakta wa sasa wa Wikimedia Foundation wanaweza kupiga kura ikiwa wameajiriwa na Wikimedia Foundation kuanzia tarehe 3 Januari 2023.

Wafanyikazi na makontrakta wa washirika wa Wikimedia

Tawi la sasa, shirika la kimuktadha, au kikundi cha watuamiaji cha wafanyikazi na makontrakta wa Wikimedia Foundation wanaweza kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kuanzia tarehe 3 Januari 2023.

Wanachama wa mashirika rasmi kama inavyofafanuliwa katika sheria ndogo za sasa za matawi ya Wikimedia, mashirika ya mada au vikundi vya watumiaji wanahitimu kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo hadi tarehe 3 Januari 2023.

Wajumbe wa bodi ya Wikimedia Foundation

Wajumbe wa sasa na wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation na Bodi ya Ushauri ya Wikimedia Foundation wanastahiki kupiga kura.

Wajumbe wa Kamati ya Harakati za Wikimedia

Wajumbe wa sasa wa Kamati za Harakati za Wikimedia wanaweza kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika majukumu hayo kuanzia tarehe 3 Januari 2023.

Waandaaji wa jamii ya Wikimedia Movement

Waandalizi wa jamii walio na hadhi nzuri, ambao hawana sifa ya kupiga kura chini ya makundi mengine, wanaweza kupiga kura iwapo watakutana na mojawapo ya yafuatayo:

 • wametuma maombi, kupokea na kuripoti angalau ruzuku moja ya Wikimedia Foundation tangu tarehe 1 Septemba 2021.
 • walikuwa waandaaji wa angalau tukio moja lililofadhiliwa la kutengeneza programu za kompyuta (hackathon), shindano au tukio lingine la Wikimedia lenye hati za kwenye wiki na angalau wahudhuriaji/wageni/washiriki 10 kati ya 3 Januari 2022 na 3 Januari 2023.

Vigezo vya Ziada

Iwapo unaona kuwa unakidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma hoja kwa ucocproject@wikimedia.org kwa barua pepe angalau siku nne kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, tarehe 27 Januari 2023 au kabla yake. Ukitimiza vigezo, tutakuongeza kwenye orodha ya wapigakura wenyewe.

Maswali ya Kawaida kuhusu Upigaji Kura

 1. Ninawezaje kuthibitisha ustahiki wangu?
  Wahariri wanaweza kutumia [zana ya Kustahiki Akaunti ya https://meta.toolforge.org/accounteligibility/65] ili kuthibitisha ustahiki katika uchaguzi wa sasa. Ukurasa wa taarifa za akaunti ya kimataifa unapatikana ili kupata maelezo zaidi kuhusu idadi ya maharirio na historia ya michango.
 2. Mahitaji ya kustahiki yamewekwaje?
  Bodi ya Wikimedia Foundation iliweka masharti ya kustahiki kabla ya kuanza kwa uchaguzi. Haya ni mahitaji yale yale yanayotumika kwa chaguzi za Bodi ya Wadhamini.
 3. Mpigaji kura anayestahiki hawezi kupiga kura
  Unaweza kupokea ujumbe: "Samahani, haupo kwenye orodha iliyotayarishwa hapo awali ya watumiaji walioidhinishwa kupiga kura katika uchaguzi huu."
  Suluhu

  Hakikisha umeingia.

  Hakikisha unapiga kura kutoka Meta-wiki, unaweza kutumia kiungo hiki kwenda kwenye ukurasa wa kuanza kupiga kura.

  Ikiwa wewe ni mstawishaji, mfanyikazi wa Wikimedia Foundation, mjumbe wa kamati ya Harakati za Wikimedia, mpokea ruzuku anayestahiki, au mjumbe wa Bodi ya Ushauri, huenda usiwe na jina mahususi la mtumiaji na utahitaji kuongezwa wewe mwenyewe kwenye orodha ya wapigakura. Unapaswa kuwasiliana na ucocproject@wikimedia.org ili kuongezwa kwenye orodha. Jibu linapaswa kutumwa ndani ya saa 72 ili kukuongeza kwenye orodha.

  Ikiwa bado unashindwa kupiga kura na unaamini unapaswa kupiga kura tafadhali acha ujumbe kwenye ukurasa wa mazungumzo wa uchaguzi au uwasiliane na Kamati ya Chaguzi kwa anwani ucocproject@wikimedia.org . Jibu linapaswa kutumwa ndani ya saa 72.

 4. Siwezi kuingia Katika VoteWiki
  Huhitaji kuingia katika VoteWiki ili kupiga kura. Ukiona kura, basi SecurePoll imefanikiwa kukutambua. Kwa sababu za usalama, ni idadi ndogo tu ya akaunti ambazo zimesajiliwa kwenye VoteWiki.
 5. Kuna mtu anaweza kuona niliyempigia kura?
  Hapana, uchaguzi ni salama. Uchaguzi huu unatumia programu ya SecurePoll. Kura ni za siri. Hakuna mtu kutoka Kamati ya Chaguzi, Bodi, wala mtu yeyote kwenye wafanyakazi wa Wikimedia Foundation anaweza kuona kura. Mwanatimu wa Imani na Usalama katika Wikimedia Foundation ana ufunguo wa usimbaji fiche kwa ajili ya uchaguzi. Baada ya ufunguo huo kuamilishwa, uchaguzi unasimamishwa.
 6. Je, ni data gani inayokusanywa kuhusu wapiga kura?

  Baadhi ya data zinazomtambulisha mtu binafsi kuhusu wapigakura zinaweza kuonekana na watu wachache waliochaguliwa wanaokagua na kujumlisha uchaguzi. Tazama wakaguzi wa uidhinishaji kama ilivyotangazwa hapo juu.

  Hii inajumuisha anwani ya IP na wakala wa mtumiaji. Habari hii hufutwa moja kwa moja siku 90 baada ya uchaguzi.

 7. Je, data hii itatumikaje?
  Takwimu kuhusu uchaguzi huu zitafupishwa kwenye matokeo ya kurasa za uchaguzi kuhusu ripoti kuu na za baada ya uchambuzi za uchaguzi. Hakuna maelezo yanayoweza kutambuliwa kibinafsi zitakazochapishwa. Maelezo haya yanayoweza kutambuliwa kibinafsi yanaweza kutumika kubaini idadi ya wapigaji kura binafsi na jinsi kura zilivyotapakaa kote ulimwenguni.
 8. Ninapopiga kura, sioni arifa yoyote kwamba kura imepokewa, na ujumbe otomatiki unatokea na kusema kwamba ninahitajika kuwa nimeingia ndani ili kupiga kura. Ni nini kinaendelea?

  Huhitaji kuingia kwenye votewiki ili kupiga kura. Hitilafu hii inawezekana ni suala la kuhifadhi. Tafadhali jaribu kupiga kura tena katika m:Special:SecurePoll/vote/394.

  Pia kumbuka kwamba uko huru kuchagua au kubadilisha chaguo lako unalopigia kura mara nyingi kadri utakavyo. Ni kura moja pekee itakayohifadhiwa kwa kila mtumiaji, na kwa urahisi mfumo utabadilisha kura yako ya zamani na kura yako mpya, na kufuta kura zozote za hapo awali.

  Wakati mchakato wako wa kupiga kura umekamilika, ujumbe wa mapokezi unaonyeshwa kwenye skrini, ambao unaweza kuhifadhi kama ushahidi kwamba umepiga kura.

 9. Mfumo wa kupiga kura umelindwa vipi dhidi ya watumiaji wanaowasilisha kura maradufu?
  Ni kura moja pekee itahifadhiwa kwenye mfumo kwa kila mtumiaji. Uko huru kuchagua au kubadilisha chaguo lako unalopigia kura mara nyingi kadri utakavyo. Kwa urahisi mfumo utabadilisha kura yako ya zamani na kura yako mpya, na kufuta kura zozote za hapo awali.
 10. Wafanyakazi wanalazimishwa au kuhamasishwa kupigia kura chaguo fulani?
  Hapana, wafanyakazi wa Wikimedia Foundation na wale wa washirika hawahamasishwi kupigia kura chaguo fulani. Tunahamasisha kila mtu binafsi kupiga kura kwa njia huru. Ili miongozo ya utekelezaji Sheria za Kinidhamu iwe fanisi, tunahitaji michango ya kweli ili kutusaidia kugundua kama kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa.
 11. Timu ya Imani na Usalama ni ya haki kuhusiana ana matokeo ya kura?
  Kitengo cha Imani na Usalama kina sehemu tatu: Sera, Maelezo Potoshi, na Operesheni. Timu inayowezesha UCoC ni timu ya Sera. Timu ya Sera haihusiki katika uchunguzi wa tabia za watumiaji. Ingawa haiaminiki kwamba timu ya Operesheni inaweza kuwa isiyo ya haki, utengenishaji huu wa majukumu uliwekwa haswa ili kuepuka hali zisizo za haki kutokea. Timu ya Sera haikadiriwi na kana kwamba hati hii iliyotengenezwa kwa ushirikiano inapitishwa kwa mara ya kwanza au marekebisho zaidi yanahitajika. Timu hii inakadiriwa na kana kwamba inashirikiana vyema na jamii. Hii inamaanisha kutengeneza mkabala wa ushirikiano wa kutekeleza UCoC ambayo inahudumia jamii. Lengo letu ni kutimiza jukumu hilo vyema kadri iwezekanavyo.
 12. Maswali mengine ambayo hayajatajwa hapa
  Kwa hitilafu za kiufundi au mfuto wa kupiga kura, tafadhali tuma barua pepe kwa anwani ucocproject@wikimedia.org. Tafadhali bainisha jina la mtumiaji ambalo unajaribu kutumia ili kupiga kura na mradi ambao unajaribu kupigia kura. Mwanatimu wa mradi atajibu barua pepe yako punde iwezekanavyo.