Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Timu ya Uratibu/Tangazo-ukumbusho wa kupiga kura

Siku za mwisho za kupigia kura Katiba ya Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language

Habarini nyote,

Ninawasiliana nanyi leo ili kuwakumbusheni kwamba kipindi cha kupiga kura kwaajili ya kuchagua Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) kitafungwa mnamo Februari 2. Wanajumuiya wanaweza kupiga kura yao na kutoa maoni kuhusu katiba kupitia SecurePoll sasa hadi Februari 2. Wale mliotoa maoni yenu wakati wa kutengeneza Mwongozo wa Utekelezaji wa UCoC mtaona mchakato huu si mgeni kwenu.

Toleo la sasa la hati ya Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili liko kwenye Meta-wiki na tafsiri zinapatikana.

Soma katiba, nenda kapige kura na uwashirikishe tangazo hili na wengine katika jumuiya yako. Ninaweza kusema kwa ujasiri kuwa Kamati ya Ujenzi ya U4C inatazamia kuona ushiriki wako.

Wako,