Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation/2023-2024/Malengo
Shirika la Wikimedia Foundation lina malengo makuu manne kwa mwaka 2023−2024. Yamesanifiwa ili kuendana na Mwelekeo wa Kimkakati wa harakati za Wikimedia na Mapendekezo ya Mkakati wa Harakati, na kuendeleza kazi nyingi zilizoainishwa katika mpango wa mwaka jana. Malengo hayo ni:
- MIUNDOMBINU: Kuboresha utoaji wa Maarifa kama Huduma Kuboresha Uzoefu wa Mtumiaji kwenye wiki, haswa wahariri mahiri. kuimarisha vipimo na kuripoti.
- USAWA: Kusaidia Usawa wa Maarifa. Kuimarisha Usawa Katika Ufanyaji Maamuzi kupitia utawala wa harakati na Mkataba wa Harakati. Kuwezesha na shirikisha harakati, kusaidia mikakati ya kikanda na saidia kuziba mapengo ya maarifa.
- USALAMA & UJUMUISHAJI: Kulinda dhidi ya vitisho vya nje vinavyoongezeka. Kutetea watu wetu na miradi dhidi ya upotoshaji wa taarifa na taratibu za serikali zenye kudhuru. Kufanya kazi katika harakati zote za Kutoa Usalama wa Watu Wajitoleaji.
- UFANISI: Kuimarisha utendaji wetu kwa ujumla. Kutathmini, Kurudia na Kurekebisha michakato yetu kwa ajili ya matokeo makubwa kwa kutumia rasimali chache zaidi.
Infrastructure |
Equity |
Safety & Inclusion |
Effectiveness |
Kupima maendeleo kuelekea kwenye malengo yetu
Ili kupima maendeleo kuelekea kwenye malengo yetu, tumetambua idadi ndogo ya vipimo vya msingi ambavyo Wikimedia Foundation inapanga kutumia katika kuleta tija kwa mwaka huu ujao. Vipimo hivi vinapaswa kuhamasisha kazi yetu na kutumika kama ishara kuashiria ikiwa tunasonga kwenye mwelekeo unaofaa. Ambapo tutakuwa hatuoni tija tunayotarajia, tutarekebisha kazi yetu ili kupata matokeo tunayohitaji.
Vipimo vya msingi vilichaguliwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo:
- Tunaamini kuwa kipimo kinaonyesha kuwa tunasonga katika mwelekeo sahihi kuelekea malengo yetu.
- Tunaamini kuwa Foundation inaweza kuwa na tija inayoweza kupimika kwenye kipimo katika kipindi cha mwaka wa fedha.
- Tunaweza kupima mabadiliko katika kipimo kila mwezi ili tuweze kusahihisha kozi inavyohitajika katika mwaka mzima wa fedha.
- Tuna uwezo wa kupima na kuweka msingi kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha.
Kwa baadhi ya matukio tulibainisha eneo muhimu la kipimo ambalo hatuna kipimo kilichoidhinishwa kisayansi au kipimo rasmicha majaribio. Kwa hali hizo, tumependekeza mitiririko ya kazi ili kuunda na kutambua vipimo katika mwaka wa fedha. Ingawa tumetambua vipimo na hatua muhimu kwa maeneo makuu ya vipimo hapa chini, kuna pointi za ziada za data ambazo Shirika litafuatilia katika mwaka ujao kwa mwonekano kamili zaidi.
Shirika la Wikimedia Foundation limebainisha maeneo makuu manne ya vipimo kwa mwaka 2023−2024.
- MAUDHUI: Kuongeza ubora na uaminifu wa maudhui ya kiensaiklopedia.
- WACHANGIAJI: Kuboresha na kudumisha afya ya jumuiya za wachangiaji wa harakati.
- UMUHIMU:Kuhakikisha umuhimu na uendelevu wetu kwa hadhira kwa upana wake duniani kote.
- UFANISI: Kuhakikisha uendelevu wetu wa muda mrefu kwa kuboresha jinsi Shirika linavyofanya kazi na kukua.
Maudhui: Kuongeza ubora na uaminifu wa maudhui ya Kiensaiklopedia.
Dhamira yetu ni kuhakikisha kuenea kwa maarifa ya bure ulimwenguni kote, na yaliyomo kwenye miradi yetu ni njia kuu ya kutoa ufikiaji wa maarifa bila malipo. Harakati zetu zimekuwa na matokeo ya ajabu kwa kiwango kikubwa na jumuiya zetu zimetumia miaka mingi kuboresha maudhui kwenye miradi yetu. Kupitia majaribio na ushirikiano, tumepata njia za manufaa za kuunga mkono juhudi zinazoendelea za jumuiya zetu ili kuongeza ubora na maudhui ya kuaminika. Lugha, maeneo na mada maeneo ambapo tunaweza kuwa na tija ni pale ambapo pia tunaboresha usawa wa maarifa bila malipo duniani kote. Kufanya kazi kwenye wiki za ukubwa wa kati ili kupanua maudhui ya kuaminika na bora, kwa ushirikiano wa karibu na watu wanaojitolea, itakuwa lengo letu kwa mwaka huu wa fedha. Metriki hii inaelekeza kwa lengo letu la kiwango cha juu la Usawa.
Kipimo: Katika wiki za ukubwa wa kati, tutaongeza asilimia ya makala za Wikipedia ambazo ziko katika maeneo ya mada yenye tija kubwa (kuanzia jinsia na jiografia) na kufikia kiwango cha ubora kinachokubalika.
Wachangiaji: Kuboresha na kudumisha afya ya jumuiya za wachangiaji wa harakati
Wafanyakazi wetu na jumuiya zinazowezesha mafanikio ya Wikipedia na ufikiaji wa kimataifa, pamoja na ufanisi wa Commons, hutuambia kuwa uendelevu wa jumuiya hizo uko hatarini. Shirika la Wikimedia Foundation lina jukumu la kusaidia kuhakikisha mafanikio na afya ya jumuiya zetu kupitia huduma za Uaminifu na Usalama, usaidizi wa usimamizi wa kujitolea, na uingiliaji kati wa kiasi ili kuongeza idadi ya wahariri. Tutafuatilia hisia za jumuiya: haswa, ni kiasi gani wanajumuiya wetu wanafurahia kushiriki na kunuia kuendelea katika harakati zetu. Pia tutazingatia ushirikiano kati ya wachangiaji ambao wanapokea usaidizi unaolengwa zaidi kutoka kwa Shirika, ikiwa ni pamoja na waandaaji, wasimamizi wa Wiki, na wachangiaji wa kiufundi. Kipimo hiki kinaonyesha malengo yetu ya kiwango cha juu cha Miundombinu na Usalama & Ujumuishaji.
Kipimo: Hatuna kipimo kilichothibitishwa ambacho kinaonyesha vyema mwelekeo wa mwaka huu kwa wahariri imara (ikiwa ni pamoja na wale walio na haki zilizoongezwa, kama vile wakabidhi, wasimamizi, wapiga doria na wasimamizi wa kila aina, pia wanaojulikana kama watendaji) na inakidhi vigezo vyetu vya kuchagua vipimo vya msingi. Badala yake, tunapendekeza lengo lenye kutupeleka mbele. Tumejitolea kutoa angalau kipimo 1 kabla ya tarehe 1 Januari 2024.
Lengo Muhimu: Kutoa uingiliaji kati mmoja muhimu kwa kila robo mwaka ambao unashughulikia vikundi hivi vya wachangiaji.
Umuhimu: Kuhakikisha umuhimu na uendelevu wetu kwa hadhira kwa upana wake duniani kote
Wikipedia ni nyenzo kwaajili ya ulimwengu kupata, kujifunza, na kushirikisha maarifa bila malipo. Sisi kwa upande wetu tunapima kwa kiasi fulani mafanikio ya kazi yetu kulingana na usomaji wetu, utumiaji tena wa maudhui yaliyoidhinishwa bila malipo, na uwezo wetu wa kuchangisha fedha ili kuendeleza malengo yetu mapana ya harakati. Harakati ya maarifa bila malipo inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kubadilisha tabia za msomaji, kutenganishwa na injini za utafutaji zinazoendeshwa na utangazaji na ukuaji wa majukwaa ya mitandao ya kijamii ambayo hutumia video na ML inayoendeshwa algorithimu za mapendekezo badala ya maandishi na wavuti wazi ili kushirikisha hadhira. Kukabiliana na changamoto hizi kunahitaji mawazo mapya katika nyanja nyingi - kuchangisha pesa, kutafuta watazamaji wapya na kujihusisha kwa ubunifu na ulimwengu unaobadilika. Metriki hii inaelekeza kwa lengo letu la kiwango cha juu la Miundombinu
Kipimo: Tutaongeza idadi ya vifaa vya kipekee kwenye Wikipedia kwa lugha na jiografia zinazolengwa.
Ufanisi: Kuhakikisha uendelevu wetu wa muda mrefu kwa kuboresha jinsi Shirika linavyofanya kazi na jinsi linavyokua.
Tuna kazi inayoendelea ya kufanya ili kuboresha masuala ya muda mrefu ya kufanya maamuzi, madeni ya kiufundi na kubainisha mkakati. Tutatayarisha vipimo vya jinsi mafanikio yatakavyokuwa tunapokuwa tunafanya kazi katika idara zote kama shirika linalofaa na lililokomaa. Metriki hii inaelekeza kwa lengo letu la kiwango cha juu la Ufanisi.
Kipimo: Hatuna kipimo kinachotambulika na kila idara itachapisha mbinu yao.