Wikimedia Community User Group Tanzania/Universal Code of Conduct

Utanguliziː

edit

Tunapenda kuwakaribisha wanajamii wote katika mjadala mahususi unaolenga kuleta baadhi ya seti ya miongozo ya tabia na mwenendo itakayotumika kuongoza na kutuhakikishia ulinzi na usalama kwa wanajumuiya wote pindi wachangiapo katika harakati na juhudi mbalimbali za shirika la WMF sambamba na hilo kuwa na mwitikio madhubuti pindi yanapojitokeza matendo ya unyanyasaji wa aina yoyote ile wakati wa uchangiaji katika miradi ya Wikimedia Foundation.

Tunapenda kuutaarifu uma waziwazi kwamba tunalenga kukusanya na kupokea maoni kutoka kwa wanajamii ili mawazo yao yatuwezeshe kuanza kufikiria kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuuunda Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili na namna utakavyoonekana.

Ni nafasi ya pekee kwa wanajumuia kushawishi namna gani mwongozo huu uweje na hakika ushiriki na michango ya wanajamii kuhusu suala hili ni maana sana kwetu.

Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili

edit

Kwa pamoja tumefikiria kuwa na ulimwengu ambao kila mwanadamu anaweza kushiriki kwa uhuru katika Jumla ya Maarifa yote. Kimsingi kila mtu anayejihusisha na harakati za shirika la Wikimedia Foundation anakuwa amejitolea kufuata maono hayo.Safari ya kuelekea kutimiza lengo hili kubwa sio kazi rahisi.

Pamoja na kwamba siku zote tumekuwa tukizingatia na kufuata viwango vya hali ya juu vya sera za maudhui kwenye miradi yetu, tumekuwa tukikumbwa na changamoto juu ya namna bora ya kutunza na kudumisha utu na udugu wakati wa uchangiaji wa maudhui katika miradi yetu.

Kumekuwa na kuibuka kwa baaadhi ya matukio ambapo baadhi ya wachangiaji wetu wamekabiliwa na dhuluma, unyanyasaji, au kuteseka kutokana na tabia za watu wengine zisizokubalika .Kutokana na mazingira hayo yasiyo rafiki, watumiaji na wachangiaji wengi wamekuwa mara kwa mara wanaacha kuchangia katika miradi yetu ya Wikimedia Foundation na hivyo tumekuwa tukikosa maarifa muhimu ambayo yangeletwa kupitia michango yao. Moja ya sababu nyingi zinazosababisha hali hiyo ni ukosefu wa miongozo elekezi ya tabia na nidhamu kwa watumiaji na wachangiaji wetu pindi wachangiapo katika miradi yetu.

Hivyo uwepo wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili unalenga kutatua mapungufu hayo. Lengo la kuwa na Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili ni kuoanisha miongozo ya tabia iliyopo tayari kwenye jumuia zetu na katika miradi mbali mbali ili kwa pamoja sasa tuunde seti ya viwango vya sera za tabia zitakazokuwa zikitumika wakati wote wa harakati za shirika la WMF.

Sera hizi zitakuwa zikitumika kwa usawa katika miradi yote, kwa wanajamii wote, na kwa wafanyakazi wote. Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili ni matokeo ya mapendekezo kuhusu harakati za Wikimedia Foundation yaliyopendekezwa na wanawikimedia na kuungwa mkono na Bodi ya Watendaji wa Wikimedia Foundation. Kila mtu atawajibika kwa usawa kudumisha tabia rafiki na fadhili kwa wengine.Hii itatusaidia sote kutengeneza mazingira ambayo maarifa ya bure yataweza kushirikishwa kwa usalama bila ya woga. Huu ni mradi mchanga unaoendelea kukua na ni mradi muhimu kwa kila moja ya miradi yetu ya Wikimedia Foundation.Mradi huu upo katika hatua za mwanzo kwa sasa, lakini hivi karibuni shirika litaanzisha mashauriano baina ya miradi ya Wikimedia Foundation kwa lugha mbalimbali. Mradi huu unategemea sana mawazo, maoni na mrejesho kutoka kwa wanajamii,hivyo basi tunawaomba na kuwahimiza sana wanajamii kushiriki katika majadiliano.

Tunaelewa kuwa ni vigumu mno kuwa na seti ya maadili ya "ulimwengu wote" itakayo kuwa wakilishi kwa tamaduni na jamii zote, lakini, inawezekana kabisa kuja na miongozo ya msingi kabisa inayoweza kuhakikisha kuwa tunakuwa na mahali salama pa kila mtu kuweza kuchangia maudhui yake katika miradi yetu. Hii ni nafasi yako ya kushawishi lugha na maudhui yatakayokuwemo katika mwongozo wa maadili, na ni fursa yako kuchangia juu ya namna bora ya kuzifanya harakati hizi zituletee mahali salama na pasipokuwa na unyanyasaji wa aina yoyote kwa wachangiaji wa miradi ya Wikimedia Foundation.

Taarifa zaidi juu ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili kwa Wanawikimedia wote (UCoC) zinapatikana hapa. Tafadhali jisikie huru kushiriki katika mijadala hata kwakutumia lugha yako uliyoizoea.

Maoni Yako

edit

Baada ya kusoma maelezo ya nia na lengo la kuwa na mwongozo wa pamoja utakao saidia kuongoza jumuia nzima ya Wanawikimedia duniani kote juu ya namna ya kujiheshimu na kuheshimu wengine wakati wa uchangiaji wa michango mbalimbali, sasa tunakukaribisha utoe maoni yako unauzungumziaje mradi huu? Unadhani una umuhimu au la? unafaa au haufai kufanyika? Jisikie huru kuelezea chochote kuhusu mradi huu. Karibu Utoe Maoni yako Hapa

Nyongeza

edit

 Tafsiri hii ya mradi wa Mwongozo wa Mwenendo kwa Wanawikimedia Duniani (Universal Code of Conduct) kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili imefanywa na  Jadnapac kwaniaba ya Wikimedia Foundation na kwaniaba ya Neha Nair (Trust & Safety Specialist, Policy (Contractor), Trust and Safety).Kwa taarifa zaidi kuhusu mradi unaweza wasiliana nae au wasiliana na Wikimedia Foundation.This translation about Universal code of Conduct from English to Swahili version has been translated by Jadnapac on behalf of Wikimedia Foundation and Neha Nair (Trust & Safety Specialist, Policy (Contractor), Trust and Safety).In case you will need  more information about this project you can reach directly to Neha Nair or the Wikimedia Foundation.