Kampeni/Timu ya Bidhaa ya WMF/Sasisho 3

This page is a translated version of the page Campaigns/Foundation Product Team/Update 3 and the translation is 100% complete.
Other languages:

Habarini nyote mliojisajili kupataJarida la taarifa za Bidhaa za Kampeni'!

Tunayo furaha kubwa kuwashirikisheni masasisho yetu:

  • Pendekezo la kuunda majina mapya ya programu: Tumependekeza kuunda majina mawili ya programu, ambazo ni "Tukio" na "Mazungumzo ya tukio." Kwa njia hii, tunaweza kuunda Kituo cha Tukio kwa urahisi ambacho huchota data kutoka kwa kurasa za tukio.Kituo hiki cha Matukio kinaweza kujumuisha zana za kuunda kurasa za matukio ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa usajili katika matukio hayo, kalenda ya matukio na takwimu za matukio ni miongoni mwa vipengele vingine vitakavyokuwepo. Muhimu zaidi, Kituo cha Tukio kitaangazia uratibu wa matukio kama sehemu muhimu ya harakati za Wikimedia. Tafadhali tushirikishe maoni yako kuhusu Phabricator au Meta kuhusu pendekezo letu la kuunda majina mawili mapya ya Programu.
  • Masasisho ya uhandisi: Tunayo furaha kubwa kwamba tumemaliza kuajiri timu yetu ya uhandisi! Wahandisi watatu na meneja wa uhandisi wamejiunga na timu yetu tangu sasisho letu la mwisho. Katika miezi michache iliyopita, wamefanya mipango ya kiufundi na kuzindua awamu ya ujenzi wa mradi huo. Sasa wanaunda zana ya usajili. Unaweza kuona timu iliyosasishwa kwenye meta.
  • Sasisho za muundo: Tulifanya majaribio ya utumiaji na kikundi kidogo cha waliojitolea kujaribu kutokana na maoni ya awali tuliyopata kuhusu mifumo ya kwenye kompyuta za mezani. Baada ya kukusanya maoni haya, tumetengeneza toleo jipya la mifumo mahususi kawaajili ya kompyuta za mezani, ambalo litakuwa tayari kushirikishwa katika wiki chache zijazo. Toleo hizi za kompyuta za mezani zinaonyesha namna mtumiaji atakavyoweza kutumia kwa mambo mawili: moja kwa waandaaji ambao wanataka kuongeza usajili kwenye kurasa zao za hafla, na nyingine kwa washiriki wanaotaka kujiandikisha kwa hafla. Zaidi ya hayo, timu ya wabunifu pia kwa sasa inashughulikia toleo la kwanza mahususi kwaajili ya simu, ambalo litashirikishwa katika kipindi cha saa ya kazi inayofuata.
1. Tazama toleo la kisasa mahususi kwaajili ya kompyuta za mezani katika Figma hapa =1472%3A36710&starting-point-node-id=1899%3A44995&show-proto-sidebar=1&hide-ui=1 Toleo la awali kwaajili ya Mratibu wa Kampeni na Usajili?node-id=1998%3A49612&scaling=min-zoom&page-id=1472%3A36710&starting-point-node-id=1998%3A49612&show-proto-sidebar=1&hide-ui=1 Usajili wa Aina ya Mshiriki.
2. tafadhali tuachie maoni yako kuhusiana na mifumo ya kwenye kompyuta za mezani. Kumbuka kuwa bado hatujachapisha toleo jipya zaidi la mifumo ya kwenye kompyuta za mezani kwenye ukurasa wa mradi, lakini tutachapisha hivi karibuni (na tafadhari jisikie huru kuongeza maoni yako kuhusu toleo lolote ambalo umeona).
  • Sasisho kuhusiana na Mabalozi: Mabalozi watatu wa bidhaa kwa jumuiya za Kiarabu, Kifaransa na Waswahili sasa wamejiunga na timu yetu! Watatusaidia kukusanya maoni kutoka kwa jumuiya za Wikimedia kuhusu mradi na kuelewa mahitaji ya waandaaji, kupitia kukusanya taarifa za moja kwa moja. Mabalozi hawa wanashiriki kama wanachama halisi wa jumuiya hizi, hivyo watatusaidia pia kutambua mahitaji ya waandaaji katika jumuiya zetu za majaribio. Mabalozi hao ni: M. Bachounda kwa jumuiya za Kiarabu, Georges Fodouop kwa jumuiya za Kifaransa, na Antoni Mtavangu kwa jamii za Waswahili.

'Kipi Kifuatacho?

Saa ya Ofisi ijayo: Tutakuwa na Lisaa Limoja tarehe 31, Machi 2022 saa 15:00 UTC, ambayo itaendeshwa kupitia /j/82046580320 Zoom. Tunakaribisha kila mtu kuhudhuria, na tunatumai sana kukuona! Lengo kuu litakuwa kwenye Zana ya Usajili. Timu pia itakuwa ikitoa masasisho ya jumuiya kuhusu matokeo ya majaribio ya utumiaji na vivutio vya muundo wa fremu za waya. Pia tutawashirikisha ratiba yetu ya sasa ya Mradi na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo. |Jiunge nasi na utushirikishe mawazo yako kuhusu maendeleo haya tuliyofanya!
Baada ya miezi michache, tunatarajia kuwa na toleo la mapema la zana yetu ya usajili linaloweza kufanyiwa majaribio. Kufikia wakati huo, timu itakuwa ikifanya awamu ya kwanza ya majaribio ya jumla na kukusanya maoni. Tunatazamia kuongeza vipengele zaidi kwenye zana kama vile usaidizi wa mawasiliano, pengine kufikia mwisho wa mwaka huu. Iwapo unajua waandaaji wengine ambao wanaweza kutaka kufuata maendeleo haya, tafadhali pendekeza kwamba jisajili kwa jarida. Tunataka kupokea maoni mengi kadri tuwezavyo.

Asante!


Timu ya Bidhaa za Kampeni