Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Timu ya Uratibu/Tangazo-Upigaji kura umefunguliwa

Pigia kura Katiba kwaajili ya Katiba ya Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language

Habarini nyote,

Ninawasiliana nanyi leo ili kuwatangazieni kwamba kipindi cha kupiga kura kwaajili ya kupata katiba ya Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) sasa kimefunguliwa. Wanajumuiya wanaweza kupiga kura yao na kutoa maoni kuhusu katiba kupitia SecurePoll sasa hadi 2 Februari 2024. Wale mliotoa maoni yenu wakati wa kutengeneza Mwongozo wa Utekelezaji wa UCoC mtakuwa tayari mnaufahamu mchakato huu.

Toleo la sasa la katiba ya Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili liko kwenye Meta-wiki na tafsiri zinapatikana.

Soma katiba, nenda kapige kura na uwashirikishe tangazo hili na wengine katika jumuiya yako. Ninaweza kusema kwa ujasiri kuwa Kamati ya Ujenzi ya U4C inatazamia kuona ushiriki wako.

Kwa niaba ya Timu ya Mradi wa UCoC,