WMDOC/Wikipedia leaflet/sw

(Redirected from Leaflet/sw)

Tafsiri ya Kiswahili:

Important note: When you edit this text, you agree to release your contribution in the public domain. If you don't want this, please don't edit.

Kamusi elezo ya wiki ni nini?

Hebu fikiria dunia ambayo kila mtu duniani ana fursa ya kupata maarifa yote duniani bila gharama yoyote. Hili ndilo linalofanyika katika kamusi elezo ya wiki. Kamusi elezo ya wiki ni kamusi elezo ya bure kabisa inayoweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale.

Mradi wa Kamusi wa Kimataifa

Mradi wa kamusi elezo ya wiki ulianza kwa lugha ya Kiingereza tarehe 15 Januari, 2001. Mradi uliofuata ulikuwa wa lugha ya Kijerumani na sasa kuna mfumuko wa kamusi elezo za wiki kwa lugha mbalimbali, Kiswahili kikiwa kimojawapo. Bado kuna jitihada za makusudi za kusisitiza sura ya kimataifa ya mradi huu. Licha ya kuwa kamusi elezo ya wiki ya Kiingereza ina zaidi ya makala 800,000 na hivyo kuwa Kamusi elezo kubwa zaidi katika mradi wa wikipedia, kuna zaidi ya makala milioni tatu kwa lugha zaidi ya 150. Nyingi ya kamusi elezo hizi za lugha mbalimbali ni kubwa na baadhi ndio zinaanza kukua.

Hakuna hajuaye kila kitu bali kila mmoja anajua kiasi/kitu fulani

Kamusi elezo ya wiki ilianza kutokana na dhana hiyo kuwa kila mtu ana maarifa fulani anayoweza kubadilishana na wenzake. Wahariri wa kamusi elezo ya wiki wana umri kati ya miaka miaka saba hadi sabini na zaidi, kila mmoja huchagia kiasi fulani cha maarifa yao na kuifanya kamusi elezo ya wiki kuwa ni zoezi la pekee duniani la elimu na maarifa shirikishi. Ni imani yetu kuwa kila mmoja ana haki ya kujifunza na pia kuwa kila mtu ana jambo analoweza (na anapaswa) kufunza wengine.

Wana jumuiya wa kamusi elezo ya wiki ni akina nani?

Katika kamusi elezo ya wiki, kila mtu ana uhuru wa kuandika, kubadili, kusahihisha, na kuhariri makala zilizomo. Kwahiyo hakuna makala zilizoandikwa na mtu mmoja pekee. Mradi huu ni shirikishi hivyo makala huweza kuandikwa na kundi la watu kumi au hata mamia. Watu wanabadilishana maarifa ya mambo wanayofahamu na kuhariri kwa pamoja ili kuweka maudhui murua katika kamusi hii. Zoezi la kuandika kamusi elezo ya wiki halina mwisho kwani kazi ya kuiboresha hufanyika kila wakati na matokeo yake ni kuwa maudhui bora zaidi hupatikana kadri siku zinavyozidi kwenda.

Wachangiaji wa kamusi elezo wanaweza kuwa na akaunti zitakazokuwa na majina yao na neno la siri, ingawa hii sio lazima. Kazi nyingi za kamusi elezo ya wiki huwekwa na watu wasio na akaunti, wengi ni wale wanaopita tu katika kamusi elezo ya wiki kusoma mambo mbalimbali na kujikuta wamechangia makala fulani kufuatia maarifa waliyonayo au kuhariri taarifa walizozikuta. Kuna kundi kubwa la watu wa aina hii ambao wanaona umuhimu wa kuendelea kuchangia maarifa baada ya kujaribu mara moja na baada ya muda mfupi wanakuwa ni sehemu ya wanajamii wa kujitolea wa kamusi elezo ya wiki. Sera yetu ya kutokuwa na ushabiki wa upande wowote imesaidia kuwezesha watu wenye historia, mtazamo, ujuzi, na uzoefu tofauti kufanya kazi pamoja. Kunapotokea mzozo tuna utaratibu wa kusuluhisha kwa amani.

“Unaweza kuhariri ukurasa huu dakika hii!”

Msingi wa mafanikio ya kamusi elezo ya wiki ugunduzi ya programu ya kompyuta iitwayo "wiki.” Programu hii iliyotengenezwa na Ward Cunningham mwaka 1995, imerahisisha utengenezaji wa tovuti mbalimbali katika intaneti zinazowezesha kila mtu kuweza kuhariri kwa urahisi na wepesi popote walipo. Kimsingi programu hii ni rahisi,ni haraka. Ndio wiki!


Wikiwiki – “haraka” kwa Kihawaii

Lugha ya wiki, inayofahamika kama wikitext, ni rahisi kuliko lugha ya kompyuta ya HTML. Kila mtu anaweza kujifunza kwa dakika chache tu. Kwa mfano, ukitaka kuweka herufi za italiki, unaweka alama hii ya nukuu: mwanzo na mwisho wa neno unalotaka liwe italiki; ukitaka kulipa neno nguvu/wino mzito unatumia alama hii ya nukuu: ' mwanzo na mwisho wa neno; na ukitaka kuweka kiungo unaweka neno unalotaka liwe kiungo ndani ya mabano haya: [[]].

Programu inayotumiwa katika kamusi elezo ya wiki inaitwa Mediawiki. Programu hii ilitengenezwa kwa nia ya kuandika kamusi elezo. Mediawiki inasambazwa kwa leseni ya General Public License (GPL) ambayo ni leseni ya programu huria inayoruhusu kila mtu kuitumia na kubadili atakavyo. Programu ya Mediawiki inatumiwa na miradi mbalimbali ingawa kamusi elezo ya wiki ndio mradi mkubwa kwa sasa.

Nawezaje kuwa mmoja wa wanafamilia wa kamusi elezo ya wiki?

Ni jambo rahisi tu, unachotakiwa kufanya kuanzia sasa ni kuingia katika ukurasa wa kamusi elezo ya wiki na kisha kuhariri taarifa mbalimbali zilizopo. Ni imani yetu kuwa utakuwa unafika katika ukurasa huo mara kwa mara na kuwa miongoni mwa watu wanaokuza mradi mkubwa kabisa wa kamusi inayoandikwa kupitia teknolojia ya intaneti.

Leseni huru ya GNU Kazi zilizopo ndani ya kamusi elezo ya wiki ziko chini ya leseni ya GNU. Hii inamaanisha kuwa kila lililomo ndani ya kamusi linaweza kutumiwa na yeyote bila kuomba ruhusa. Pia inamaanisha uhuru wa kuhariri, kunakili, na kusambaza kuendana na leseni.

Miradi shirikishi ya Wikipedia

Kutokana na kukua kwa kamusi elezo ya wiki, miradi shirikishi ilianzishwa ili kusaidia uboreshaji wa maudhui ya kamusi elezo ya wiki. Baadhi ya miradi hii imekua na kuweza kusimama kama miradi pekee igawa bado ipo katika familia ya kamusi elezo ya wiki na kuna mahusiano ya moja kwa moja ya kila siku kati ya miradi hii na mradi mama. Baadhi ya miradi hii ni pamoja na:

Wiki Kamusi Mradi wa Kamusi huru katika lugha mbalimbali: http://www.wiktionary.org

Wiki vitabu Mradi unaolenga utoaji wa masomo mbalimbali kwa wasomaji: http://www.wikibooks.org

Wikinukuu Sehemu huru ya kufanyia nukuu mbalimbali: http://wikiquote.org

Wiki vyanzo Mradi wa vyanzo vya taarifa mbalimbali: http://www.wikisource.org

Wiki Habari Taarifa za matukio mbalimbali zilizoandikwa na watu mbalimbali(ambao sio lazima wawe waandishi wa habari): http://www.wikinews.org

Wikimedia Commons Mkusanyiko wa picha na mafaili mengine mbalimbali (kama video, muziki, n.k.) yanayopatikana bure: http://commons.wikimedia.org

Taasisi ya Wikimedia

Taasisi ya Wikimedia, yenye makao yake makuu Florida, Marekani, ni shirika mama la kamusi elezo ya wiki na miradi mingine iliyotajwa hapo juu. Imesajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali lenye nia ya kusambaza maarifa bure kwa kila mtu duniani. Taasisi hii inagharamia mradi huu.

Hivi sasa kamusi elezo ya wiki ni moja ya tovuti 50 mashuhuri duniani.

Je ninawezaje kusaidia?

Taasisi ya Wikimedia inategemea michango ya watu mbalimbali kuendesha miradi yake. Kama unapenda kuona kamusi elezo ya wiki na miradi mingine inaendelea kukua, unaweza kuchangia kupitia teknolojia za mtandaoni za PayPal au MoneyBookers. Jina la akaunti yetu ni: donation@wikipedia.org. PayPal inaruhusu uchangiaji wa mara moja,au kila mwezi, au hata kila mwaka. Kwa taarifa zaidi nenda katika ukurasa huu: http://wikimediafoundation.org/wiki/Fundraising.

Unaweza kuchangia kupitia anuani ya Posta

Unaweza pia kuchangia kwa kutumia posta. Tuma mchango kwa ofisi kuu ya Wikimedia iliyoko katika anuani hii:

Wikimedia Foundation Inc.
200 2nd Ave South, #358
St. Petersburg, FL 33701-4313

Kama unatuma fedha toka nje ya Marekani, tutafurahi ukituma kwa hawala ya fedha ya kimataifa au hundi inayokubalika na benki za Marekani ili kuepuka gharama za kupata fedha hizo. Tafadhali usitume fedha taslimu kwa njia ya posta.


English