Maangazo ya Wikimedia, Juni 2012

This page is a translated version of the page Wikimedia Highlights, June 2012 and the translation is 100% complete.

Maangazo kutoka kwa Ripoti ya Wakfu wa Wikimedia na Ripoti ya Uhasibu wa Wikimedia ya Juni 2012, na chaguo za matukio mengine ya maana kutoka kwa harakati ya Wikimedia

Maangazo ya Wakfa wa Wikimedia

Kundi la ushauri lajadili muundo wa kusambaza fedha wa baadaye

 
Mkutano wa kikundi cha washauri wa FDC wafanyika huko San Francisco

Juni 9-10 kundi la ushauri kwa ajili ya kuundwa kwa Kamati ya Usambazaji Fedha (FDC) siku zijazo walikutana katika ofisi za Wakfu huko San Francisco. Jumuiya ya wahanga, Wadhamini wa Wikimedia, wawakilishi wa sura, wafanyakazi wa wakfu na wanachama wa Kundi la Bridgespan walijadili jinsi FDC itaongoza maamuzi juu ya usambazaji wa fedha (zaidi ya $ 10,000,000 katika 2012-13) kati ya Wakfu, sura na makundi mengine. Kulingana na mapendekezo, Bodi ya Wadhamini imepitisha mkataba na utendaji kazi wa awali wa FDC. Wana Wikimedia ambao wanataka kutumikia FDC wana alikwa nominate|kujiteua wenyewe.

 
Alama ya mradi chombo cha kuhariri

mfano wa pili wa Visual Editor wazinduliwa

Mfano mpya wa "Visula Editor" ya mirado ya Wikimedia ulizinduliwa, toleo la kwanza ambalo linaweza ku tengeneza kurasa na kuhariri kurasa. Itawezesha watumiaji kuchangia bila ya kujifunza wikitext syntax ngumu.

Majaribio ya "Teahouse" yahitimisha kwa matokeo ya kutia moyo

Teahouse, ambapo wahariri wapya wa Wikipedia wanaweza kupata msaada kutoka kwa wanachama wenye uzoefu wa jamii ya Wikipedia, ilihitimisha awamu ya miezi yake ya mitatu ya majaribio kwenye Wikipedia ya Kiingereza, kuchapisha ripoti na vipimo. Wahanga 568 walijitolea kushiriki katika majaribio. Katika utafiti, asilimia 70% walisema kuwa waliliridhika na Teahouse, wakati asilimia 5% tu walisema hawakuridhika.Wahariri wapya ambao walikuwa wamealikwa kwa Teahouse walifanya hariri nyingi baadaye zaidi ya wale ambao hawakupata mwaliko. Asilimia 28 ya washiriki wa Teahouse ni wanawake, ikilinganishwa na asilimia 9 ya wahariri wote kwa Wikipedia kwa ujumla.

Hackers wakutana huko Berlin

 
Picha ya panorama ya hackathon huko Berlin

Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchi 30 walienda Berlin kwa Berlin Hackathon, iliyondaliwa na Wikimedia Ujerumani na Wakfu.Walikuwa ni pamoja na watengenezaji MediaWiki, watumiaji wa Toolserver, watawala mifumo, waandishi wa bot na wasimamizi, waumbaji Gadget, na wanateknolojia wengine wa Wikimedia. Jamii pia ilijifunza zaidi juu ya miradi ya Wikidata na RENDER.

Takwimu na Mwelekeo

Wageni wa kipekee wa Mei:

Milioni 492.39 (+4.02% ikilinganishwa na April, +19.79% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
(takwimu ya comScore ya miradi yote ya Wakfu wa Wikimedia; comScore itatoa takwimu za Juni baadaye mnamo Julai)

Maombi ya Kurasa ya Juni:

bilioni 18.1 (+0.2% ikilinganishwa na Mei; +22.7% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
(logi ya takwimu ya seva, Miradi yote ya Wikimedia ikijumuishwa na wanaopata kwa njia ya simu)

Wahariri waliosajiriwa wa Mei 2012 (>=5 hariri/mwezi)

85,200 (+0.38% ikilinganishwa na Aprili / +3.25% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
(Takwimu za hifadhidata, miradi yote ya wakfu wa Wikimedia isipokuwa Wikimedia Commons). Ilani: Katika siku chache zijazo, tutahamia kigezo ambacho kinazingatia Sul na Wikimedia Commons.

Ripoti Kadi (kuunganisha takwimu mbalimbali na mwelekeo juu ya miradi ya WMF) ya Mei 2012:

http://reportcard.wmflabs.org/

Fedha

 
Mapato na matumizi ya Mwaka hadi sasa ya Wakfu wa Wikimedia ikilinganishwa na mpango wa Mei 31, 2012
 
Matumizi ya fedha ya Mwaka hadi sasa ya Wakfu wa Wikimedia kama ilivyo Mei 31, 2012

(Habari ya fedha inapatika tu hadi Mei 2012 kwa wakati huu wa ripoti hii.)

Habari yote ya fedha iliyo wasilishwa ni ya kipindi cha Julai 1, 2011 - Mei 31, 2012.

Mapato $ 35,563,497
Matumizi:
 Kikundi cha Teknolojia $ 10,979,122
 Jamii/Kikundi cha Kuchangisha Fedha $ 3,612,603
 Kikundi cha Ukuaji Duniani kote $ 3,882,629
 Kikundi cha Utawala $ 863,259
 Fedha/Kisheria/Raslimali Watu/Kikundi cha Usimamizi $ 6,127,792
Jumla ya Matumizi $ 25,465,405
Jumla ya mabaki/(hasara) $ 10,098,092
  • Mapato ya mwezi ni $659K ikilinganishwa na mpango wa $162K, kwa kukadiria $497K ama 306% juu ya mpango.
  • Mwaka-hadi-sasa ni $35.6MM ikilinganishwa na mpango $29MM, ikikadiriwa ni $6.6MM ama 23% juu ya mpango.
  • Matumizi ya mwezi ni $3.4MM ikilinganishwa na mpango wa $2.2MM, kwa kukadiria ni $1.2M ama 50% zaidi ya mpango, kwa sbabau ya kufiki capital expenditures
  • Mwaka kufikia sasa ni $25.5MM ikilinganishwa na mpango $25.7MM, ikikadiriwa $252K ama 1% chini ya mpango.
  • Nafasi ya fedha ni $29.1MM mnamo May 31, 2012 - ikikadiriwa ni miezi 12.5 ya matumizi.

Maangazo mengine ya Harakati

"Afripedia" yaleta Wikipedia iliyo nje ya mkondo katika sehemu za mashinani za Africa

Mpango huo mpya unaoitwa "Afripedia" unafanya Wikipedia kunapatikana katika maeneo ya Afrika Magharibi ambapo hakuna muunganisho mzuri wa mtandao. Mradi utasanikisha (Kiwix) matoleo ya Wikipedia yaliyo nje ya mkondo katika flash. Hizi zitawekwa katika kompyuta ndogo, zisizo na skrini au keyboards(plug kompyuta) ambazo zimeshikanishwa na mtandao wa ndani wa WiFi. Mtu yeyote ambaye anapata ishara ya WiFi atakuwa na uwezo wa kupata maudhui. Mradi huu ni ushirikiano wa Wikimedia Ufaransa na Agence de la Francophonie universitaire (Shirika la Vyuo Vikuu la Francophonie - AUF) naInstitut français (IF). Hii itaanza katika vyuo vikuu 20 katika nchi 15 za Afrika Magharibi.

 

Mkutano wa pili wa "Ibeoconf" kufanyika huko Santiago de Chile

Mwishoni mwa wiki ya kwanza ya Juni, Mkutano wa pili wa Ibero-American Wikimedia (ujulikanao kama "Iberoconf") ulifanyika huko Santiago de Chile.ulihudhuliwa na wawakilishi wa sura za Wikimedia za Argentina, Bolivia,Brazil, Chile, Colombia, Italia, Mexico, Ureno, Uhispania, Uruguay and Venezuela, na wageni kutoka Panama, Peru, Wakfu wa Wikimedia na Wikimedia Ujerumani.

"Chuo cha Wikipedia" juu ya utafiti kuhusu Wikipedia

Mwishoni mwa Juni, "Shule ya Wikipedia 2012" ilileta pamoja watafita wa akademia na wana Wikimedia huko Berlin, iliyoandaliwa na Wikimedia Ujerumani.Haswa utafiti kuhusu Wikipedia na kuhusu maarifa bure kwa kijumla kwa mkutano huu.Makaratasi mbalimbali na video yanapatikana mtandaoni.

Mkutano wa kila mwezi wa wakfu wa Wikimedia wa vipimo na shughuli uliofanyika manmo Julai 5, 2012 ulizingatia mpango wa mwaka wa 2012-13 badala ya kuzingatia Juni kama ilivyo desturi. Video iliyorekodiwa itapakuliwa kwa commons wakati wa uchapishaji wa Mpango wa Mwaka.